MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 8, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 8, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

SOMO 1

Mwa. 28:10-22

Yakobo alitoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulanl akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.

Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamisha juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama. malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.

Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli, Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 91 :1-4, 14-15 (K) 2

(K) Mungu wangu nitakayemtumaini.

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini. (K)

Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,
Na katika tauni iharibuyo.
Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao. (K)

Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua jina langu.
Ataniita nami nilamwitikia;
NitaKuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza. (K)

SHANGILIO

Lk.8:15

Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu
na wema wa mioyo yao,
hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.

INJILI

Mt. 9: 18-26

Yesu alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.

Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu, imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama. Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote.

Neno la Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Maisha ya Mtoto Yesu huko Nazareth yanatufundisha nini?

Yanatufundisha kuishi kwa uaminifu, kufuata malezi bora, kuwatii wazazi, walezi na wakubwa zetu. (Lk 2:51, Rum 13:1).. soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 8, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 8, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa Malaika Mlinzi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kando ya mito ya babeli

[Tafakari ya Sasa] 👉Njia ya Kumrudia Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Teresa (Teresia) wa Yesu (Avila)

UJUMBE-HONGERA-NDUGUU.JPG

a.gif Kwa nini ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo?

Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila tunapofanya ukumbusho wa sadaka hiyo pekee tunazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu “ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yoh 13:1)... soma zaidi

a.gif Ni fadhila gani inayoondoa majivuno?

Fadhila inayoondoa majivuno ni fadhila ya Unyenyekevu.. soma zaidi

a.gif Je, ni muhimu tujiandae kufa?

Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Eb 9:27)… soma zaidi

a.gif Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kufanya nini?

Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila ya mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua… soma zaidi

a.gif Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;.. soma zaidi

a.gif Tumuadhimishe nani?

Tumuadhimishe Mungu pekee siku zote za maisha yetu kwa tumaini la kumuadhimisha milele… soma zaidi

a.gif Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Uaminifu

Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu… soma zaidi

a.gif Malaika wema kazi yao ni nini?

Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika wetu Walinzi. (Ebr 13:2).. soma zaidi

a.gif Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.