MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 22, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SIKUKUU YA MT. MARIA MAGDALENA

SOMO 1

Wim. 3 :1-4

Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate. Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini, Katika njia zake na viwanjani, Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate. Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! mmemwona mpendwa wa nafsi yangu? Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

Au

SOMO 1

2 Kor. 5 :14-17

Upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.

Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena, Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab 63: 1-5, 7-8 (K) 1

(K) Nafsi yangu inakuonea kiu, Ee Bwana.

Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. (K)

Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu. (K)

Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. (K)

Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
Nafsi yangu inakuandama sana;
Mkono wako wa kuume unanitegemeza. (K)

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Maria tuambie: sema uliyoona njiani.
Kaburi lilimfadhi yule aliye Mzima;
Niliona utukufu wa Kristu alipokuwa akifufuka.
Aleluya.

INJILI

Yn. 20 :1-2, 11-18

Siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka

Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka. Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. Yesu akamwambia, Mama unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.

Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (yaani, Mwalimu wangu). Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani… soma zaidi

a.gif Je, divai (pombe) ni halali?

Ndiyo, divai ni halali, mradi itumike kwa kiasi isije ikaleta madhara… soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu hutajwa wapi katika Rozari?

Roho Mtakatifu hutajwa katika fungu la tatu la Matendo ya Utukufu tusemapo; Aliyepeleka Roho Mtakatatifu. (Mdo 2:1-4).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 22, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 22, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala ya Malaika w Bwana

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kando ya mito ya babeli

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni Mwaminifu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Getrudi Mkuu

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG

a.gif Kazi ya Upadre ni ya kipekee

UPADRE NI KAZI YA PEKEE YA HEKIMA, UWEZO NA MAPENDO YA UMUNGU WA KRISTU. KAMWE USIMSHAMBULIE PADRE. "Yesu Maria na Yosefu nawapenda, ziokoeni Roho. KUMTETA PADRE [Haya ni maelezo ya Bwana wetu kwa Mutter Vogel.] " Kamwe mtu asimshambulie Padre hata anapokuwa katika makosa badala yake umwombee na fanya toba ili niweze kumpa tena NEEMA… soma zaidi

a.gif Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake nini?

Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake ni kwamba, kabla hajazaliwa kama mtu duniani ni Mungu, sawa na Baba anayemzaa yeye tu tangu milele… soma zaidi

a.gif Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13).. soma zaidi

a.gif Biblia inavyomshauri mwanaume Kuhusu mke wake

Mpende mke wako mzuri
Usimkaripie mke wako ukiwa unaongea nae. Inamuumiza sana.
Mithali 15:1.. soma zaidi

a.gif Katika amri ya kwanza ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa kumdharau Mungu na kuweka imani yetu katika viumbe badala ya Mungu… soma zaidi

a.gif Je, kuna viumbe ambavyo tunaviheshimu kwa kumtukuza Mungu?

Ndiyo twamuheshimu Bikira Maria, Malaika na Watakatifu… soma zaidi

a.gif MIUJIZA NA MATOKEO YA MUNGU NA WATAKATIFU

Ingiza kichwa cha habari cha Muujiza au matokeo hapa chini kwenye kaboksi kisha bofya mbele yake.. soma zaidi

a.gif Kwa njia ya watawa Kanisa linaonyesha nini mbele ya watu wote?

Kanisa linaonyesha jinsi Yesu alivyotenda mahali popote pale alipopita kwa mfano wagonjwa, maskini, wakosefu, watoto, vilema, wenye njaa na wasiojua habari njema.. soma zaidi

a.gif Katika Amri ya Nane Mungu anaamuru nini?

Katika Amri ya Nane Mungu anaamuru tuseme ukweli na tulinde heshima ya wengine. (Mt 5:37, Yak 5:12)… soma zaidi

a.gif UZURI NA WITO WA MAISHA YA NDOA NA FAMILIYA

Katika ulimwengu wa leo tunashuhudia changamoto nyingi za ndoa zinazoleta hisia hasi za vijana na wale ambao hawajajifungamanisha na fumbo hili takatifu. Ni wazi changamoto zipo lakini haziwezi kufifisha au kuondoa uzuri na utakatifu wa maisha ya ndoa na familiya… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.