MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 15, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Kanisa linahusika vipi na imani?


MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 15, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

SOMO 1

Kut. 1:8-14,22

Aliinuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi, tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, kukitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii, Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali. Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtahifadhi hai

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 124 (K) 8

K: Msaade wetu u katika jina la Bwana.

Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi,
Israeli na aseme sasa,
Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi
wanadamu walipotushambulia.
Papo hapo wangalitumeza hai,
Hasira yao ilipowaka juu yetu. (K)

Papo hapo maji yangalitugharikisha,
Mto ungalipita juu ya roho zetu.
Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu
Maji yafurikayo. (K)

Na ahimidiwe Bwana:
Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno hayo.
Nafsi yetu imeokoka kama ndege
Katika mtego wa wawindaji,
Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. (K)

SHANGILIO

1 Sam. 3:9 Yn. 6:68

Aleluya, aleluya,
Nena Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia:
wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.

INJILI

Mt. 10:34 - 11:l

Yesu aliwafundisha mitume wake: Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipomimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.

Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

Neno la Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana… soma zaidi

a.gif Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi… soma zaidi

a.gif Adhimisho la Liturujia Hutumia Ishara na Alama zipi?

Adhimisho la Liturujia Hutumia Ishara na Alama zinazohusiana na uumbaji, maisha ya binadamu na historia ya wokovu; nazo ni;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 15, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 15, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA BWANA

[Wimbo Mzuri PA.gif] Salamu Mama Mwema

[Tafakari ya Sasa] 👉Kukosa hata mara moja inahesabika ni kukosea

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Teresa (Teresia) wa Yesu (Avila)

a.gif Ujumbe wa leo

*UJUMBE WA LEO*
Ndege anapokuwa hai huwa anakula sana funza, lakini atakapokufa nae huliwa na funza.. Maisha yanabadilika kila wakati, usimdharau wala kumuumiza mtu yeyote katika maisha…Unaweza ukawa imara sana leo lakini kumbuka maisha ni imara kuliko wewe.., Mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima….. soma zaidi

a.gif Mambo gani yanavunja amri ya kwanza ya Mungu?

Mambo hayo ni;.. soma zaidi

a.gif Mafuta ya mpako wa wagonjwa yanamaanisha nini?

Mafuta ya wagonjwa yanamaanisha lengo la kuwaponya na kuwarudishia nguvu na uzuri… soma zaidi

a.gif Yesu amemweka nani kuwa mkubwa wa Kanisa?

Yesu amemweka Mtume Petro kuwa Mkubwa wa Kanisa zima. (Mt 16:18-19). Halifa wa Mtume Petro ni Baba Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ni nini?

Ni Sakramenti ambayo Padri humuombea neema ya Mungu na kumpaka Mafuta Matakatifu mgonjwa aliye katika hatari ya kifo kwa ajili ya neema ya roho na mwili. (Yak 5:14-15, Mk 6:13).. soma zaidi

a.gif Moyo Mtakatifu wa Yesu unawakilisha nini?

Moyo Mtakatifu wa Yesu unawakilisha Upendo na Huruma ya Mungu isiyo na mipaka… soma zaidi

a.gif Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?

Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo.. soma zaidi

a.gif Pamoja na kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume, mtu anapewa kipaimara vipi?

Pamoja na kuwekea mikono na mwandamizi wa Mitume, mtu anapewa kipaimara kwa kupakwa krisma kama mhuri wa kuwa mali ya Bwana. Ndiyo inayotufanya tuitwe Wakristo nyuma ya Yesu aliyeitwa Kristo… soma zaidi

a.gif Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu kwa sababu tunapaswa kutumia kwa utukufu wake vipawa alivyotujalia, kama vile vya kujenga, kupamba, kuchonga, kuchora na kucheza. Kwa njia hizo tutokeze na kukoleza imani yetu na ya wenzetu… soma zaidi

a.gif Kutafuta dhambi maana yake ni nini?

Kutafuta dhambi maana yake ni kujiuliza moyoni dhambi nilizotenda Tangu ungamo la mwisho (Ef 4:17-32).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.