MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 1, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Wokovu unapatikana wapi?

Somo la Kwanza

Mwa 18:16-33

Watu hao waliondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize. Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.

Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.

Wimbo wa katikati

Zab 103:1-4, 8-11

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
(K) Bwana amejaa huruma na neema.

Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema,
(K) Bwana amejaa huruma na neema.

Bwana amejaa huruma na neema,
Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Yeye hatateta sikuzote,
Wala hatashika hasira yake milele.
(K) Bwana amejaa huruma na neema.

Hakututenda sawasawa na hatia zetu,
Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.
(K) Bwana amejaa huruma na neema.

Somo la Injili

Mt 8:18-22

Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng'ambo. Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako. Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu. Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.


a.gif Sala ya Baba yetu

Inasaliwa Hivi;.. soma zaidi

a.gif Nguvu ni nini?

Ni moyo wa kushika sana Amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu, matukano, mateso wala kufa. (Rum 8:38-39).. soma zaidi

a.gif Zifahamu dhambi ambazo huondolewa na PAPA pekee au Padre kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu

ZIFAHAMU DHAMBI AMBAZO HUONDOLEWA NA PAPA PEKEE AU PADRE KWA MAMLAKA MAALUMU KUTOKA KWA PAPA :.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 1, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 1, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA MATUMAINI

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Karoli Lwanga

UJUMBE-ZA-USIKU-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Uaminifu

Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu… soma zaidi

a.gif Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?

Ndiyo, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele… soma zaidi

a.gif Kila Mwanadamu anaye Malaika wake wa kumlinda?

Ndiyo, Kila Mwanadamu anaye Malaika wake wa kumlinda ndiye Malaika Mlinzi. (Mt. 18:10).. soma zaidi

a.gif Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?

Ndiyo, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. Yesu alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso… soma zaidi

a.gif Umwilisho maana yake ni nini?

Umwilisho ni ile hali ya Yesu kama Mungu kujifanya mtu kwa Bikira Maria mzaa. (Yoh 1:14).. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa wapi?

Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa kwenye Tabernakulo.. soma zaidi

a.gif Je kuna aina tofauti ya dhambi?

Ndiyo, kuna dhambi za mawazo, maneno, matendi na kutotimiza wajibu… soma zaidi

a.gif Tuwaonaje Wakristo ambao sio Wakatoliki?

Ingawa wamejitenga katika ushirika kamili wa Kanisa Katoliki, tunawatambua kuwa ndugu zetu kutokana na ubatizo wao… soma zaidi

a.gif Hagari na Ishmaeli (Mtoto wa kwanza wa Abrahamu alivyopatikana)

1 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri… soma zaidi

a.gif Umoja wa Mungu unategemea nini?

Umoja wa Mungu unategemea hasa kwamba Mwana na Roho Mtakatifu wanachanga Umungu wa Baba, ambaye wanatokana naye pasipo utengano wowote. Baba anajifahamu na kujipenda: wazo analojifahamu ndiye Mwana, upendo anaojipenda katika wazo hilo ndiye Roho Mtakatifu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.