MASOMO YA MISA, JUMATATU, AGOSTI 5, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMATATU, AGOSTI 5, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

SOMO 1

Hes. 11 :4-15

Wana wa Israeli walilia wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hi; mana tu.

Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtarna, na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola. Watu wakazunguka-zunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga kwa mawe ya kusagia, au kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa nyunguni, na kuandaa mikate; na tamaa yake ilikuwa kama tamu ya mafuta mapya. Umande ulipoyaangukia marago wakati wa usiku, hiyo mana ilianguka pamoja nao.

Basi Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za Bwana zikawaka sana; Musa naye akakasirika.

Musa akamwambia Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako? kwa nini sikupata neema machoni pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu? Je! ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote? je! ni mimi nilivewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto aamwaye, wende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao? Nipate wapi nyama ya kuwapa watu hawa wote? kwani wanililia, wakisema, Tupe nyama, tupate kula. Mimi siwezi kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda. Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie mbali, kwamba nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka yangu.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 81 :11-16 (K) 1

(K) Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha.

Watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu,
Wala Israeli hawakunitaka.
Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao,
Waenende katika mashauri yao. (K)

Laiti watu wangu wangenisikiliza,
Na Israeli angeenenda katika njia zangu;
Ningewadhili adui zao kwa upesi,
Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu. (K)

Wamchukiao Bwana wangenyenyekea mbele zake,
Bali wakati wao ungedumu milele.
Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano,
Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani. (K)

SHANGILIO

Zab. 119:34

Aleluya, aleluya,
Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.

INJILI

Mt. 14: 13-21

Yesu aliposikia habari ya kuuawa kwa Yohane Mbatizaji, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka miiini mwao. Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu. akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi kula. Wakamwambia, Hatuna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. Akasema, Nileteeni hapa.

Akawaagiza makutano wakati katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Tafakari: Je tunamkumbuka Mungu wakati gani?

Msimamizi wa ujenzi alikuwa anamwita mjenzi chini ya jengo yeye akiwa ghorofa ya 16. Lakini kwa sababu ya kelele za nje, mjenzi pale chini hakusikia sauti hiyo… soma zaidi

a.gif Ni ishara gani zinazoshuhudia ufufuko wa Yesu?

Ni ishara zifuatazo;.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa inaadhimishwaje?

Inaadhimishwa kwa Padre kumuombea mgonjwa, kumuwekea mikono na kumpaka mafuta katika panda la uso na viganja vya mikono; kwa kutumia mafuta aliyobariki Askofu siku ya Alhamisi kuu… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATATU, AGOSTI 5, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATATU, AGOSTI 5, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Majitoleo

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nipeleke Mbinguni Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa siku zote

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Karoli Lwanga

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

waliokufa-zaman-wapo-wap.JPG

a.gif Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti huenda wapi?

Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti hutupwa motoni milele. (Mt 25:41).. soma zaidi

a.gif Je magoti yanayopigwa wakati mwingine tofauti na wakati wa kuabudu yana maana gani?

Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwa Mkao wa sala.. soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Uzima wa milele

Maswali na majibu kuhusu uzima wa milele;.. soma zaidi

a.gif Habari njema kwa watu wote maana yake ni nini?

Maana yake ni;.. soma zaidi

a.gif Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu… soma zaidi

a.gif Mungu ametufunulia nini?

Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu… soma zaidi

a.gif Kanisa linatoa visakramenti kwa nani?

Kanisa linatoa visakramenti hata kwa waamini wenye vizuio na kwa wasio Wakristo, kwa sababu vinaeleweka na kuthaminiwa kwa urahisi, kwa kuwa zinasaidia kufurahia maisha… soma zaidi

a.gif Je, Biblia zote ni sawa?

Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza… soma zaidi

a.gif Makala mpya kwa sasa

Makala Mpya ni kama ifuatavyo,.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.