MASOMO YA MISA, JUMATANO, JUNI 26, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

Somo la Kwanza

Mwa 15: 1-12, 17-18

Neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana Mungu, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu. Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. Kisha akamwambia, mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi ili uirithi. Akasema, Ee Bwana Mungu nipateje kujua ya kwamba nitairithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, Na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akawaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua. Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia. Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama. Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati

Wimbo wa katikati

Zab 105:1-4,6-9

Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake,
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
uapo wake kwa Isaka.
(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Shangilio

Zab 147 : 12, 15

Aleluya, aleluya,
Msifu Bwana, ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.

Somo la Injili

Mt 7:15-20

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.


a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki, Namna ya Kuwa na Amani

Namna pekee ya kuwa na Amani ni kuishi Mapenzi ya Mungu,.. soma zaidi

a.gif Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?

Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo.. soma zaidi

a.gif Ufalme wa simu wa sasa

➡ Asubuhi saa 12 : 00 mtu anaamka, kabla hata HAJAMUSHUKURU MUNGU, kabla hata hajatoka kitandani, kabla hata hajajifunua shuka,.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATANO, JUNI 26, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATANO, JUNI 26, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Malkia wa Mbingu

[Wimbo Mzuri PA.gif] Karoli - Nipe Biblia

[Tafakari ya Sasa] 👉Tumaini kwa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Fransisko wa Asizi

JE-MARIA-NI-MAMA-YETU-PIA.JPG

a.gif Wakati wa kwaresma yawapasa waamini kufanya nini?

Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa;.. soma zaidi

a.gif Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?

Hapana, si mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote, bali mengine yanahitaji mhudumu wake awe amepewa daraja inayoshirikisha uwezo ambao Yesu aliwapa Mitume wake.

“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Lk 6:12-13)… soma zaidi

a.gif Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20).. soma zaidi

a.gif Padri anaondolea dhambi mahali pa nani?

Padri anaondolea dhambi mahali pa Mungu.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Mungu alitupa Amri kumi?

Mungu alitupa amri kumi ili kutufudisha mambo yatupasayo kwa Mungu, kwa watu na kwetu sisi wenyewe.. soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba… soma zaidi

a.gif Kisa cha Noa na Wanawe

18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani… soma zaidi

a.gif Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa lini?

Yesu alitimiliza Agano la Kale kwa namna isiyotarajiwa hasa aliposulubiwa, akionekana na Wayahudi wenzake kama kwamba amelaaniwa:.. soma zaidi

a.gif Agano la Tohara

1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu… soma zaidi

a.gif Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.