MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 31, 2019: JUMA LA 17 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

SOMO 1

Kut. 34 : 29-35

Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na ztie mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling’aa kwa sababu amesema na Bwana. Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling’aa; nao wakaogopa kumkaribia. Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao.

Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote ambayo Bwana amemwambia katika mlima Sinai. Na Musa alipokuwa amekwisha kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake. Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za Bwana kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa. Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling’aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 99: 5-7, 9 (K)9

(K) Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.

Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu,
sujuduni penye kiti cha miguu yake, ndiye mtakatifu. (K)

Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,
na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake,
walipomwita Bwana aliwaitikia. (K)

Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao.
Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa. (K)

Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu,
sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu,
maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu. (K)

SHANGILIO

Yak 1:18

Aleluya, aleluya, Kwa kupenda kwake mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake. Aleluya.

INJILI

Mt. 13 :44-46

Yesu aliwaambia makutano mifano, Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Ili Askofu atoe ruhusa ya kufungisha ndoa ya mchanganyiko au dini tofauti kuna Masharti gani?

Ndiyo, Askofu atatoa ruhusa baada ya Mkristo Mkatoliki kuahidi kwamba;.. soma zaidi

a.gif Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > “hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42)… soma zaidi

a.gif Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu Anatutakasa?

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa njia ya Sakramenti, Visakramenti, Fadhila za Kimungu na vipaji vyake. (Yoh 16:8).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 31, 2019: JUMA LA 17 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 31, 2019: JUMA LA 17 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TISA

[Wimbo Mzuri PA.gif] Moyo safi wa Mama Maria

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Ambrosi

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG

a.gif Katika mwaka wa kanisa tunakumbuka nini?

Katika Mwaka wa Kanisa tunakumbuka natunaadhimisha matukio na mafumbo yote ya ukombozi wetu na hivyo twapata neema zake.. soma zaidi

a.gif Dhamiri adilifu ni nini?

Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Malaika

Mambo ya Msingi kujua kuhusu Malaika;.. soma zaidi

a.gif Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti huenda wapi?

Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti hutupwa motoni milele. (Mt 25:41).. soma zaidi

a.gif Nafasi ya Mateso katika maisha

Ni kwa nini tunapata Mateso na shida katika Maisha? Kwa nini Mungu ameruhusu tuteseke?.. soma zaidi

a.gif Biblia iliandikwa kwa kusudi gani?

Biblia iliandikwa kusudi tupate “kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini” tuwe “na uzima wa milele” (Yoh 20:31)… soma zaidi

a.gif Dhambi nyepesi hutupotezea nini?

1. Hudhoofisha upendo ndani mwetu
2. Huzuia Maendeleo ya roho zetu kwa kuzuia fadhila na kutenda mema… soma zaidi

a.gif Kuzaliwa kwa Isaka

1 Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema… soma zaidi

a.gif Wakati wa kwaresma yawapasa waamini kufanya nini?

Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa;.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ni nini?

Sakramenti ni ishara wazi ionekanayo ya neema isiyoonekana, iliyofanyizwa kwanza na Yesu Kristu mwenyewe; ilete neema au izidishe neema moyoni mwetu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.