MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 3, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SIKUKUU YA MTAKATIFU TOMA, MTUME

SOMO 1

Efe. 2:19-22

Tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 117 (K) Mk. 16:15

(K) Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili.

Aleluya.
Enyi mataifa wote, mhimidini.
enyi watu wote, mhimidini. (K)

Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu,
na uaminifu wa Bwana ni wa milele. (K)

SHANGILIO

Yn. 20 : 29

Aleluya, aleluya, Wewe, Tomaso, kwa kuwa umeniona, umesadiki, wa heri wale wasioona, wakasadiki. Aleluya.

INJILI

Yn. 20 :24-29

Mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako, uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu; wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.

Injili ya Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Injili ni nini?

Injili ni Habari njema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo.. soma zaidi

a.gif Dhambi ya asili ndio nini?

Dhambi ya asili ambayo binadamu wote wanazaliwa nayo, ni hali ya kukosa utakatifu na hali ya asili ya urafiki na Mungu.. soma zaidi

a.gif Vizuizi vya ndoa ni kitu gani?

Vizuizi vya ndoa ni vile vinavyofanya ndoa isiwe halali tangu mwanzo.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 3, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 3, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TANO

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mkono wako wa kuume

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa KiMungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Justin mfiadini

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

KADI-MZAZI-ASUBUHI.JPG

a.gif Nani atenda dhambi dhidi ya Amri ya tatu ya Mungu?

Anayetenda dhambi dhidi ya amri ya tatu ya Mungu ni yule:-.. soma zaidi

a.gif Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka 'Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina'… soma zaidi

a.gif Baada ya kujua maisha ya Yesu tunapaswa kufanya nini?

Baada ya kujua maisha ya Yesu tunapaswa kujilinganisha naye hadi aundwe na kuishi ndani mwetu akitushirikisha uhai, kifo na ufufuko wake… soma zaidi

a.gif Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;

  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani?

Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani ili abebe kwa upendo na kufidia dhambi za watu wote, alivyotabiriwa:.. soma zaidi

a.gif Adhabu za dhambi huondolewa kwa namna gani? Jinsi ya kupata rehema

Adhabu za dhambi huondolewa kwa;
1. Kufanya malipizi au majuto kamili
2. Kuvumilia taabu na mateso katika maisha
3. Kuvishinda vishawishi na majaribu.. soma zaidi

a.gif Usafi wa Moyo ndio nini?

Usafi wa Moyo ni fadhila ya kiutu, zawadi ya Mungu, neema na tunda la Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Mashauri ya Injili ni nini?

Ni mwaliko wa kuchagua kwa hiari kuishi;
1. Ufukara
2. Utii
3. Ubikira au usafi kamili kwa ajili ya ufalme wa Mungu (Mk 10:29-30).. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Mawazo na Mipango ya Mungu kwa mtu

Mungu daima anawaza Mema na Anampangia Mtu Mambo mema… soma zaidi

a.gif Katika amri ya pili ya Mungu tumekatazwa nini?

Katika amri ya pili ya Mungu tunakatazwa kuapa bure kwa Jina la Mungu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.