MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 8, 2019 DOMINIKA YA 23 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Hek. 9:13 – 19

Ni mtu yupi awezaye kulijua shauri la Mungu? Au ni nani atakayeelewa na mapenzi yake? Kwa kuwa mawazo ya wanadamu yana woga, na makusudi yetu yanaelekea kushindwa; na mwili wenye uharibifu huigandamiza roho, na kiwiliwili cha kidunia huzilemea akili zilizosongwa na masumbuko. Kwa shida tu twayapambanua yaliyoko duniani, na yaliyo karibu nasi ni kazi kuyaona; lakini yaliyoko mbinguni ni nani aliyeyagundua? Naye ni yupi aliyeyavumbua mashauri yako, isipokuwa ulimpa Hekima na kumpelekea Roho yako takatifu kutoka juu? Ndivyo miendo yao wakaao duniani ilivyosafishwa, na wanadamu walivyofundishwa yakupendezayo; hata na kwa Hekima wao wenyewe waliponywa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 90:3 – 6, 12 – 14, 17 (K)1

(K) Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.

Wamrudisha mtu mavumbini,
Usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
Maana miaka elfu machoni pako
Ni kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na kama kasha la usiku. (K)

Wawagharikisha, huwa kama usingizi,
Asubuhi huwa kama majani yameayo.
Asubuhi yachipuka na kumea,
Jioni yakatika na kukauka. (K)

Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie moyo wa hekima.
Ee Bwana, urudi, hata lini?
Uwahurumie watumishi wako. (K)

Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,
Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.
Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu.
Na kazi ya mikono yetu uithibitishe. (K)

SOMO 2

Flm. 9 – 10, 12 – 17

Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia. Nakusihi kwa ajili ya motto wangu niliyemza katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo; niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa; ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili. Lakini sikutaka kutenda neno lolote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari. Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; tokea sasa, si kama mtumwa, bali Zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana; na kwako wewe Zaidi sana, katika mwili na katika Bwana. Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Efe. 1:17 , 18

Aleluya, aleluya,
Ewe Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
Uyatie nuru macho ya mioyo yetu,
Ili tujue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo.
Aleluya.

INJILI

Lk. 14:25 – 33

Makutano mengi walipokuwa wakifuatana na Yesu, yeye aligeuka, akawaambia, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume kwa wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyo alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za Amani, mtu yule akali mbali. Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Je, Roho Mtakatifu Katika mfano wa ndimi za Moto Maana yake nini?

Maana yake ni kupata nguvu ya Kuhubiri Injili, Neno la Mungu linalopenya kwenye Moyo Kama Moto… soma zaidi

a.gif Ibada ni nini?

Ni roho ya kupenda utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na Heshima.. soma zaidi

a.gif Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 8, 2019 DOMINIKA YA 23 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 8, 2019 DOMINIKA YA 23 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala ya Baba yetu

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mtazameni Mkombozi

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Agostino wa Hippo

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG

a.gif Faida ya kuabudu Ekaristi Takatifu

1.Kila saa moja tunayotumia kuabudu, inafurahisha moyo wa Yesu na hivyo majina yetu huandikwa mbinguni kwa ajili ya uzima wa milele (Mama Thereza wa Calcuta).. soma zaidi

a.gif Tafakari: Je tunamkumbuka Mungu wakati gani?

Msimamizi wa ujenzi alikuwa anamwita mjenzi chini ya jengo yeye akiwa ghorofa ya 16. Lakini kwa sababu ya kelele za nje, mjenzi pale chini hakusikia sauti hiyo… soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana… soma zaidi

a.gif Sakramenti zipi ni kwa ajili ya huduma kwa jamii na kanisa?

Sakramenti zilizowekwa kwa ajili ya huduma kwa jamii na Kanisa ni Daraja Takatifu na Ndoa… soma zaidi

a.gif Tumejuaje kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu?

Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA

Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake… soma zaidi

a.gif Kwa nini Mungu alitupa Amri kumi?

Mungu alitupa amri kumi ili kutufudisha mambo yatupasayo kwa Mungu, kwa watu na kwetu sisi wenyewe.. soma zaidi

a.gif Je, Yesu alirudia maisha ya duniani?

Hapana, Yesu hakurudia maisha ya duniani: tofauti na watu aliowafufua warudie maisha haya, Yesu mfufuka ameshaingia utukufu wa milele:.. soma zaidi

a.gif Hasira ni nini?

Hasira ni kukasirika bure kuonea na kulipiza kisasi.. soma zaidi

a.gif Viumbe vyenye hiari ni vipi?

Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.