MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 29, 2019 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 29, 2019 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA

SOMO 1

Amos. 6:1, 4 – 7

Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria; ninyi mnaolala juu ya vitanda vya pembe, na kujinyosha juu ya masemadari yenu; ninyi mnaokula wanakondoo wa kundi, na ndama waliomo zizini; ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu. Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani, na kelele za machezo za hao waliojinyosha zitakoma.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 146: 6 – 10 (K) 1

(K) Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.

Bwana huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa.
Huwapa wenye njaa chakula,
Bwana hufungua waliofungwa. (K)

Bwana huwafumbua macho waliopofuka,
Huwainua walioinama.
Bwana huwapenda wenye haki,
Huwahifadhi wageni. (K)

Bwana huwategemeza yatima na mjane,
Bali njia ya wasio haki huipotosha.
Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. (K)

SOMO 2

1Tim. 6:11 – 16

Wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utawa, Imani, upendo, saburi, upole. Piga vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi. Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa. Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.

SHANGILIO

Yn. 17:17

Aleluya, aleluya,
Neno lako ndiyo kweli,
Ee Bwana; Ututakase sisi kwa ile kweli.
Aleluya.

INJILI

Lk. 16:19 – 31

Yesu aliwaambia Mafarisayo, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, WAsipowasikia Musa na manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Je, utawala wa Yesu umeshaanza?

Ndiyo, utawala wa Yesu umeshaanza nao utakamilika atakaporudi kuwahukumu wazima na wafu kwa kutenganisha moja kwa moja wema na wabaya… soma zaidi

a.gif Ni wakati gani katika Misa Mkate na Divai vinageuka Mwili na Damu yake Kristo?

Ni katikati ya Misa padri asemapo maneno Matakatifu aliyosema Yesu mwenyewe: "HUU NDIO MWILI WANGU; HII NDIO DAMU YANGU".. soma zaidi

a.gif Maana ya jina Bikira Maria

Jina asili kwa Kiaramu ni מרים, Maryām lenye maana ya "Bibi"; watafsiri wa kwanza wa Biblia ya Kiebrania wanaojulikana kama Septuaginta (LXX) waliliacha kama lilivyo wakiandika kwa Kigiriki Μαρίαμ, Mariam, au walilifupisha wakiandika Μαρία, Maria… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 29, 2019 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 29, 2019 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu yupo kwa ajili yako

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Jorome

MLO-MWEMA-KWA-NDUGU-UJUMBE.JPG

a.gif Kwa kugusa kifua tuna maana gani?

Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni… soma zaidi

a.gif Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?

Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote… soma zaidi

a.gif Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba nini?

Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba Mbingu na dunia, na viumbe vingine vingi vyenye kuonekana mimea na watu. (Mwanzo 1;31).. soma zaidi

a.gif Nini maana ya Roho Mtakatifu?

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26).. soma zaidi

a.gif Mkusanyo Sheria Kanuni za Kanisa unaelezaje kuhusu Makatekista?

Unaeleza kuwa - Makatekista ni Walei Wakristo ambao wamepewa malezi halisi na wanajitokeza vizuri katika maisha ya Ukristo wao… soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidi

a.gif IBADA YA HURUMA KUU YA MUNGU

Habari njema ni kwamba Yesu sasa anakuja kwako Kama Bwana wa Huruma, Mwalimu na Rafiki Mwema Akupendaye, Angalia Usichelewe Wakati akija Kama Hakimu asikukute bado huna ushirika nae na hujui haki na hukumu yake. Wakati ndo huu wa kukimbilia Huruma na Upendo wake wa Bure Kwako... soma zaidi

a.gif Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?

Hapana, ubatizo uliotolewa na Yohan Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu, mwanzilishi wa sakramenti zote… soma zaidi

a.gif Kwa nini tunasali na Kumuabudu Mungu?

Je unasali kwa hofu ya kutokua na uhakika na maisha?.. soma zaidi

a.gif Je, ubatizo tuu unatosha?

Hapana, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.