MASOMO YA MISA JUMAPILI, OKTOBA 6, 2019 DOMINIKA YA 27 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA JUMAPILI, OKTOBA 6, 2019 DOMINIKA YA 27 YA MWAKA

SOMO 1

Hab. 1:2 – 3; 2:2 – 4

Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi asana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia; ingojee; kwa kuwa haina bidi kuja, haitakawia. Tazama, roho yake hujivunia, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa Imani yake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 95:1 – 2, 6 – 9, (K) 7 – 8

(K) Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo yetu.

Njoni tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele yake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi. (K)

Njoni, tuabudu tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi, tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake. (K)

Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu;
Kama huko Meriba;
Kama siku ile ya Musa jangwani,
Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu. (K)

SOMO 2

2Tim. 1:6 – 8; 13 – 14

Ndugu yangu, nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu nay a upendo nay a moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wal ausinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu. Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika Imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Yn. 15:15

Aleluya, aleluya,
Ninyi nimewaita rafika,
kwa kuwa yote niliyoyasikia
kwa baba yangu nimewaarifuni.
Aleluya!

INJILI

Lk. 17:5 – 10

Mitume walimwambia Bwana, Tuongezee Imani. Bwana akasema, Kama mngekuwa na Imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.

Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? Je! Atampa asante yule mtumwa; kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Yatupasa nini kwa wenye Daraja Takatifu?

Yatupasa
1. Kuwaheshimu.. soma zaidi

a.gif Mambo gani yanavunja amri ya kwanza ya Mungu?

Mambo hayo ni;.. soma zaidi

a.gif Mafundisho ya dini kuhusu Marehemu

Kuhusu Marehemu;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA JUMAPILI, OKTOBA 6, 2019 DOMINIKA YA 27 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA JUMAPILI, OKTOBA 6, 2019 DOMINIKA YA 27 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nimekukimbilia

[Tafakari ya Sasa] 👉Tumaini kwa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

biblia-kuhusu-kifo.JPG

a.gif Tuwaheshimu Baba na Mama kwa matendo gani?

Tuwaheshimu Baba na Mama kwa matendo ya adabu, heshima, utii na mapendo (Ayu 3:12).. soma zaidi

a.gif Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu… soma zaidi

a.gif Amani ya Moyoni au Rohoni

Amani ya Moyoni au Rohoni ni hali ya kutokua na wasiwasi na hofu moyoni kuhusu Mambo ya Rohoni na ya kidunia… soma zaidi

a.gif Dhambi nyepesi ni nini?

Dhambi nyepesi ni kosa la kuvunja Amri ya Mungu au ya Kanisa katika jambo dogo, au jambo kubwa kwa makusudi yasiyo kamili. (1 Yoh 5:17).. soma zaidi

a.gif Yesu maana yake nini?

Yesu maana yake ni “Mungu Mwokozi”: alichaguliwa jina hilo kabla hajazaliwa, akitabiriwa kuwa “yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Math 1:21)… soma zaidi

a.gif Amri kumi za Mungu ni zipi?

1. Ndimi Bwana, Mungu wako usiabudu miungu wengine.
2. Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
3. Fanya siku ya Mungu.. soma zaidi

a.gif Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?

Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi.. soma zaidi

a.gif Muamuzi wa Mwisho ni Mungu

Mungu ndiye Muamuzi;.. soma zaidi

a.gif Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51

Hii ndiyo Sala ya Toba;.. soma zaidi

a.gif MPANGILIO WA KURASA ZA POSTI NA MAKALA

Makala kuu za Wakatoliki;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.