MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 27, 2019 DOMINIKA YA 30 YA MWAKA C WA KANISA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 27, 2019 DOMINIKA YA 30 YA MWAKA C WA KANISA

MWANZO

Zab. 105:3-4

Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. Mtakeni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.

SOMO 1

YbS. 35:12 – 14, 16 – 19

Kwa kuwa Bwana ndiye mhukumu wala hakijali cheo cha mtu. Hatamkubali yeyote juu ya maskini, naye ataisikiliza sala yake aliyedhulumiwa. Hatayadharau kamwe Malalamiko ya yatima, wala ya mjane amwelezapo habari zake. Malalamiko yake aliyeonewa yatapata kukubaliwa, na dua yake itafika hima mbinguni. Salsa yake mnyenyekevu hupenya mawingu; wal ahaitatulia hata itakapowasili; wala haitaondoka hata Aliye juu atakapoiangalia, akaamua kwa adili, akatekeleza hukumu. Wala Bwana hatalegea, wala hatakuwa mvumilivu kwa wanadamu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 34: 1 – 2, 16 – 18, 22 (K) 6

(K) Maskini huyu aliita Bwana akasikia.

Nitamhimidi Bwana kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie wakafurahi. (K)

Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Ili aliondoe kumbukumbu lao duniani.
Walilia, naye Bwana akasikia.
Akawaponya na taabu zao zote. (K)

Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
Bwana huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao. (K)

SOMO 2

2Tim. 4:6 – 8, 16 – 18

Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda: baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote, pia waliopenda kufunuliwa kwake. Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

SHANGILIO

Yn. 8:12

Aleluya, aleluya!
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.

INJILI

Lk. 18:9 – 14

Yesu aliwaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma;p hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Mafundisho kuhusu Hukumu ya Mwisho

Maswali na majibu kuhusu hukumu ya mwisho;.. soma zaidi

a.gif Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?

Hapana, ubatizo uliotolewa na Yohan Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu, mwanzilishi wa sakramenti zote… soma zaidi

a.gif Kila kitu ni mali ya Mungu isipokua hiki

Kila kitu ni mali ya Mungu. Kuwa na Mungu ni kuwa na kila kitu. Hata mimi mwenyewe ni mali ya Mungu. Kitu kimoja tu nina hakika nacho kwamba ni mali yangu binafsi nacho ni dhambi zangu😛. Ee Mungu naomba niziungame niweze kubaki mali yako bila kuwa na kitu binafsi... soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 27, 2019 DOMINIKA YA 30 YA MWAKA C WA KANISA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMAPILI, OKTOBA 27, 2019 DOMINIKA YA 30 YA MWAKA C WA KANISA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA BWANA

[Wimbo Mzuri PA.gif] Karoli - Nipe Biblia

[Tafakari ya Sasa] 👉Uhuru na Amani ya Moyoni

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Gemma Galgani

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

a.gif Je, Kanisa ni kundi la binadamu tu?

Hapana, Kanisa si kundi la binadamu tu, tunaloweza kulianzisha kama vile chama, timu n.k… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya kwanza daima ni ipi?

Sakramenti ya kwanza daima ni ubatizo, kwa kuwa ndio kupata uzima mpya kwa kushiriki kifo na ufufuko wa Yesu, inavyodokezwa wazi zaidi mtu akizamishwa na kutolewa majini… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa sababu gani

Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa ajili ya watu wote hasa wagonjwa.. soma zaidi

a.gif Usafi wa Moyo ndio nini?

Usafi wa Moyo ni fadhila ya kiutu, zawadi ya Mungu, neema na tunda la Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Sadaka ya Msalaba ni nini?

Sadaka ya Msalaba ni tendo la mateso na kifo cha Bwana wetu Yesu Kristojuu ya Msalaba pale Kalvari.. soma zaidi

a.gif Vichwa au Mizizi ya dhambi ni ipi?

1. Majivuno
2. Uchoyo
3. Wivu
4. Hasira
5. Tamaa mbaya
6. Ulafi
7. Uvivu au uzembe.. soma zaidi

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Yesu aliweka sakramenti ngapi?

Yesu aliweka sakramenti saba ambazo ni;
1. Ubatizo (Yoh 3:3, Mk. 16:15-16)
2. Kipaimara (Isa 11:2, Mdo 8:14-17)
3. Ekaristi Takatifu (Yoh 6:1-7, 1Kor 11:24-25)
4. Kitubio (Mt 16:18-19; 18:18; Yoh 20:21-23)
5. Mpako Mtakatifu (Mk 6:13, Yak 5:14-15)
6. Daraja Takatifu (Lk 22:21-25; 1Kor 11:24-25)
7. Ndoa (Mwa 2:21-25; Mt 19:3-9).. soma zaidi

a.gif Watu wa jinsia moja waweza kuoana?

Hapana, watu wa Jinsia moja hawawezi kuoana na wakifanya hinyo wanatenda dhambi kubwa inayomlilia Mungu. (Wal 18:22).. soma zaidi

a.gif Katika Amri ya kwanza ya Kanisa tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusikilize Misa kila siku ya Mungu na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.