MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 25, 2019 DOMINIKA YA 21 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 25, 2019 DOMINIKA YA 21 YA MWAKA

SOMO 1

Isa 66: 18-21

Bwana asema hivi, Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu. Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi. Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema Bwana.

Neno la Bwana…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 117 (K) Mk 16: 1512

(K) Enendeni ulimwenguni mwote, Mkaihubiri Injili..

Aleluya.
Enyi mataifa yote, msifuni Bwana,
Enyi watu wote, mhimidini. (K)

Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu,
Na uaminifu wa Bwana ni wa milele. (K)

SOMO 2

Ebr 12: 5-7, 11-13

Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi. Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.

Neno la Bwana…Tumshukuru Mungu

SHANGILIO

Yn. 17: 17

Aleluya, aleluya,
Maneno yako ndiyo kweli, Ee Bwana, Ututakase sisi kwa ile kweli.
Aleluya.

INJILI

Lk. 13: 22-30

Yesu alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha katika safari yake kwenda Yerusalemu. Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. Naye atasema, Nawaambia, siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu. Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.

Neno la Bwana…Sifa kwako, Ee Kristo


a.gif Ijue Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa paji la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka 'Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina'… soma zaidi

a.gif Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?

Maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo kwa sababu yanafafanua ishara nyingine na kuzitia nguvu ya kututakasa… soma zaidi

a.gif Mtakatifu Mathayo Mtume

Mathayo (kwa Kiebrania מַתִּתְיָהוּ, Mattityahu au מתי, Mattay, Zawadi ya Mungu; kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa hasa kutokana na Injili yenye jina lake. Labda aliitwa pia Lawi… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 25, 2019 DOMINIKA YA 21 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 25, 2019 DOMINIKA YA 21 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala ya Asubuhi ya kila siku

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mahali pazuri - UPENDO

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala inayojibiwa

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu John Fisher

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

UJUMBE-WA-SHUKRANI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Mafundisho na mapokeo Katika Kanisa Katoliki yanapopatikana kwenye Biblia

JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?.. soma zaidi

a.gif Kifungu cha Biblia kinachothibitisha kua Bikira Maria Mama wa Yesu ni Mama wa Wakristu Wote

Kwa ufupi.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya neno la Mungu Luka 16

Tafakari ya Leo;.. soma zaidi

a.gif Kitubio tupewacho na padre chatosha?

Ni shida kutosha. Mara nyingi chataka malipizi ya hapa duniani kama kufunga, magonjwa, masumbuko, sala n.k mateso yasipotosha hapa duniani yatakamilishwa toharani.. soma zaidi

a.gif DOMINIKA YA UTATU MTAKATIFU

Ni sikukuu ambayo Huazimishwa baada ya Jumapili ya Pentecoste kwa kufuata Dogma ya Kanisa juu ya Utatu Mtakatifu, Ni watu watatu ktk Mungu Mmoja , yaani Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,.. soma zaidi

a.gif Chagua kunyamaza: Huu ni ushauri kwa Leo

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi

a.gif Mungu aenea pote maaana yake ni nini?

Mungu aenea pote maaana yake yupo kila mahali mbinguni na duniani wala hakuna mahali asipokuwepo?. (Zab, 139:7-12).. soma zaidi

a.gif Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?

Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la… soma zaidi

a.gif Mambo makubwa yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika

Zifuatazo ni sababu kubwa za msingi zinzozifanya ndoa nyingi za kizazi cha Leo kuvunjika haraka na kukosa kudumu.. soma zaidi

a.gif Watawa wanashika mashauri gani ya Kiinjili?

Watawa wanashika hasa mashauri ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu ambayo msingi wake ni maisha na mafundisho ya Yesu kadiri ya Injili… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.