MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 18, 2018 DOMINIKA YA 20 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, divai (pombe) ni halali?

SOMO 1

Yer. 38:4 – 6, 8 – 10

Ndipo wakuu walimwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari. Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lolote kinyume chenu. Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo. Ebedmeleki akatoka nyumbani mwa mfalme, akamwambia mfalme, akisema, Ee Bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hapana mkate kabisa katika mji. Ndipo mfalme akamwamuru Ebedmeleki, Mkushi, akisema, chukua pamoja nawe watu thelathini; toka hapa, ukamtoe Yeremia shimoni, kabla hajafa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 40:1 – 3, 17 (K) 13

(K) Ee Bwana, unisaidie hima

Nalimngoja Bwana kwa saburi,
Akaniinamia akakisikia kilio changu. (K)

Akanipandisha toka shimo la uharibifu,
Toka udongo wa utelezi;
Akaisimamisha miguu yangu mwambani,
Akaziimarisha hatua zangu. (K)

Akatia wimbo mpya kinyani mwangu,
Ndiyo sifa zake Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa,
Nao watamtumaini Bwana. (K)

Nami ni maskini namhitaji,
Bwana atanitunza.
Ndiwe msaada wangu na wokovu wangu,
Ee Mungu wangu, usikawie. (K)

SOMO 2

Ebr. 12:1 – 4

Sisi pia kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini sana yeey aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Lk. 19:38

Aleluya, aleluya,
Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; Amani mbinguni, na utukufu huko juu.
Aleluya.

INJILI

Lk. 12:49 – 53

Siku ile Yesu aliwaambia makutano: Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi? Lakini nina ubatizo unipasao kubatizwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe?

Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano. Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe; mkwe na mkwe mtu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Watoto wawili wa Adamu na Eva walkikuwa wepi?

Walikuwa ni Kaini na Abeli.. soma zaidi

a.gif Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;.. soma zaidi

a.gif MIUJIZA NA MATOKEO YA MUNGU NA WATAKATIFU

Makala za Miujiza… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 18, 2018 DOMINIKA YA 20 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 18, 2018 DOMINIKA YA 20 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Siri ya Imani kwa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Bakhita

MLO-MWEMA-KWA-NDUGU-UJUMBE.JPG

a.gif Kanisa ni Katoliki maana yake ni nini?

Kanisa ni Katoliki maana yake ni la watu wote mahali pote na nyakati zote… soma zaidi

a.gif Utawala wa Yesu umeanza hasa wapi?

Utawala wa Yesu umeanza hasa katika Kanisa lake linalokusanya wale waliomuamini kuwa ni Bwana wakaokolewa… soma zaidi

a.gif Mafundisho kuhusu Vilema, Vichwa vya dhambi au mizizi ya dhambi

Kuhusu vilema au vichwa vya dhambi soma haya;.. soma zaidi

a.gif Misa ni nini?

Misa ni sadaka safi ya Wakristo kwa Mungu, ndiyo sadaka ya Agano Jipya ambayo
Kristo kwa njia ya Padri anamtolea Mungu Baba mwili na damu yake katika umbo la mkate na divai kama alivyojitolea mwenyewe juu ya msalaba… soma zaidi

a.gif Kwa nini ubatizo unafanyika kwa maji?

Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo ishara ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Bikira Maria ni nani? Mambo makuu ya kushangaza usiyoyajua kuhusu Bikira Maria

Mpendwa msomaji, mara nyingi umekuwa ukijiuliza mengi kuhusu Bikira Maria. Leo nimekukusanyia maswali na majibu kuhusu mambo muhimu ambayo ungependa kuyajua kuhusu Bikira Maria kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Mungu ajua yote maana yake nini?

Mungu ajua yote maana yake ajua ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu.. soma zaidi

a.gif Picha ya Huruma ya Mungu

Bwana Yesu alianza kumtokea Sista Faustina mfululizo tangu mwaka 1930 hadi 1938. Alimtokea ili kumwandaa kwa ujumbe mkubwa wa maisha wa kuitgazia dunia nzima ibada ya Huruma ya Mungu, ambayo ilikuwa na madhumuni yafuatayo;

  • Kuandaa ujio wa Pili wa Bwana wetu Yesu Kristo aliye Mfalme wa Huruma.
  • Kuokoa roho zilizoko Toharani.
  • Kuwaongoa wakosefu ambao wameshapoteza neema ya kujiombea.
  • Kuitangaza Huruma ya Mungu… soma zaidi

a.gif Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu… soma zaidi

a.gif Je, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya mwamba?

Ndiyo, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya Mtume Petro, alichunge lote kwa niaba yake. Papa kama Askofu wa Roma ndiye mwandamizi wa Petro na mkuu wa kundi zima la Maaskofu, waandamizi wa Mitume… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.