MASOMO YA MISA, JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019: DOMINIKA YA 19 YA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019: DOMINIKA YA 19 YA MWAKA C

Somo la Kwanza

Hek 18:6-9

Usiku ule baba zetu walitangulia kuonywa, ili wakiwa na ufahamu hakika, wafurahishwe na viapo walivyovitegemea; kwa hiyo watu wako waliutazamia wokovu wa wenye haki na uharibifu wa adui. Madhali uliwalipia kisasi watesi wale, na kwa njia ile ile uliwatukuza ukituita ili tukujie. Zaidi ya hayo watoto watakatifu wa watu wema walitoa dhabihu kwa siri, na kwa moyo mmoja walijitwalia agano la torati ya dini, ya kwamba watashirikiana katika mambo mema na vile vile katika hatari; pindi walipoimbisha nyimbo takatifu za mababu katika kumhimidi Mungu.

Wimbo wa katikati

Zab 33:1, 12, 18-16,20-22

Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.
Watu aliowachagua kuwa urithi wake.

(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.

Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojea fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa.

(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.

Nafsi zetu zinamngoja Bwana,
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivvokungoja Wewe.

(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao.

Somo la Pili

Ebr 11:1-2, 8-19

Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana Ibrahimu aiipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenlni katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika. Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; Naam. yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.

Shangilio

Yn 8:12

Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. asema Bwana: Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.

Somo la Injili

Lk 12:32-48

Yesu aliwaambia makutano: Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Viuzeni mlivyo navvo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa. akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu. Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu. Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; nanyi iweni kama watu wanaomng jea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwa- karibisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwa kuta hivi, heri watumwa hao. Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi; angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu. Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia? Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, arnbaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, arnbaye bwana wake ajapo atamkuta anafanva hivyo. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini. Na mtumwa yule aliye jua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, nave amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.


a.gif Elimu ni nini?

Ni maarifa ya kutambua werevu na udanganyifu wa shetani; anaposhawishi mwenyewe au kwa kutumia vitu au watu. (1Pet 5:8-9).. soma zaidi

a.gif Yesu aliweka makanisa mangapi? Yesu hakufanya makanisa mengi?

Hapana. Yesu alifanya Kanisa moja tuu… soma zaidi

a.gif Matokeo ya hukumu hiyo ni nini?

Matokeo ya Hukumu hiyo ni roho kwenda Mbinguni, Toharani au Motoni. (Mt 25:34-46).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019: DOMINIKA YA 19 YA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019: DOMINIKA YA 19 YA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Bwana ndiwe mwenye haki

[Tafakari ya Sasa] 👉Kumtafuta Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Margareta Maria Alacoque

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

SASA.gif

a.gif Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu lini?

Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo Yesu ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote… soma zaidi

a.gif Anayebatizwa yampasa nini?

Yampasa kuungama imani yake ama mwenyewe akiwa mtu mzima ama kupitia wazazi kama akiwa mtoto mdogo.. soma zaidi

a.gif Kanisa kuwa takatifu maana yake nini?

Kanisa kuwa takatifu maana yake ni kazi ya Mungu mtakatifu inayong’aa katika watakatifu wa mbinguni, hasa Bikira Maria… soma zaidi

a.gif Dhambi ya mauti ni nini?

Dhambi ya Mauti ni kosa la kuvunja Amri ya Mungu au ya Kanisa, katika jambo kubwa, kwa fahamu na kusudi. (1 Yoh 5:16).. soma zaidi

a.gif Mungu ni Mkubwa

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake. "Baba, hivi Mungu ni mkubwa kiasi gani?" Baba yake akatazama juu angani akaona ndege ya abiria akamuuliza mwanae "mwanangu, ile ndege ina ukubwa Gani?" Mtoto akajibu ni ndogo sana.
Basi Baba yake akamchukua hadi uwanja wa ndege walipofika karibu na ndege akamuonesha ndege akamuuliza " ile ndege ina ukubwa gani?? Mtoto akajibu "Hiyo Ndege ni Kuuuubwa sana" basi Baba yake akamwambia.. soma zaidi

a.gif Yesu alitukomboa kwa hatua zipi?

Yesu alitukomboa kwa Hatua Mbili (2) ambazo ni;.. soma zaidi

a.gif Je, tuishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo?

Hapana, tusiishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo, kwa kuwa imani na sakramenti zinadai kutekelezwa maishani… soma zaidi

a.gif Neema ya Msaada ni nini?

Neema ya Msaada ni msaada tupatao kwa Roho Mtakatifu kutuongezea nguvu Rohoni tutende mambo mema na tuepuke Mabaya.. soma zaidi

a.gif Nani anatenda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu? Mambo yanayovunja Amri ya Tano ya Mungu

Anayetemda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu ni yule;-.. soma zaidi

a.gif Kutokumuabudu Mungu ni kwa namna gani?

Ni kuruhusu kitu chochote kimtawale mtu badala ya Mungu, mfano cheo, pombe, mali, shetani, tuisheni, kazi, na kutoadhimisha Jumapili au kutoshiriki… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.