MASOMO YA MISA, JUMANNE, SEPTEMBA 17, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMANNE, SEPTEMBA 17, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA

SOMO I

1 Tim 3: 1-13

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.

Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu. wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.

Neno la Bwana…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 100: 1-3, 5-6

(K.) Nitakwenda kwa unyofu wa moyo

Rehema na hukumu nitaziimba,
Ee Bwana, nitakuimbia zaburi.
Nitaiangalia njia ya unyofu;
Utakuja kwangu lini? (K.)

Nitakwenda kwa unyofu wa moyo
Ndani ya nyumba yangu.
Sitaweka mbele ya macho yangu
Neno la uovu. (K.)

Amsingiziaye jirani yake kwa siri,
Huyo nitamharibu.
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,
Huyo sitavumilia naye. (K.)

Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
Hao wakae nami.
Yeye aendaye katika njia kamilifu,
Ndiye atakayenitumikia. (K.)

SHANGILIO

Lk 7:16

Aleluya, aleluya,
Nabii mkuu ametokea kwetu;
na Mungu amewaangalia watu wake.
Aleluya.

INJILI

Lk. 7:11-17

Yesu alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye. Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. Habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote, na katika nchi zote za kando kando.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Usidanganyike Binti yangu

Binti mmoja alitaka ushauri kutoka kwa Mwalimu na maongezi yao yalikuwa hivi.. :
🔹 Binti : Shallom mwalimu..
🔹 Mwl : Shallom maranatha, binti yangu.
🔹 Binti : Mwl, kuna swali naomba nikuulize, maana linanisumbua sana kichwa changu.
🔹 Mwl : usijal binti yangu, karibu.
🔹 Binti : Mwl, mimi ni binti niliyeokoka na nampenda YESU, nina mchumba wangu ninampenda sana na yeye ananipenda pia, lakini yeye hajaokoka. Sasa ninaweza kuwa nae? Tuna malengo ya kuoana… soma zaidi

a.gif Je, Tunawajibika kwa dhambi zilizotendwa na wengine?

Ndiyo, Tunawajibika kwa dhambi zilizotendwa na wengine iwapo tunazichangia kwa kutenda kosa husika… soma zaidi

a.gif Mungu ni nani? Sifa za Mungu

Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote, katika mbingu na nchi, Mkubwa wa Ulimwengu mwenye kuwtunza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya. (Mt: 6:8-9, Yoh 20: 17).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMANNE, SEPTEMBA 17, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMANNE, SEPTEMBA 17, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala ya Asubuhi ya kila siku

[Tafakari ya Sasa] 👉Jambo la muhimu zaidi Duniani

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Anna

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

BIKIRA-MARIA-NI-MALKIA-WA-KIPEPEO.JPG

a.gif Misa ni nini?

Misa ni sadaka safi ya Wakristo kwa Mungu, ndiyo sadaka ya Agano Jipya ambayo
Kristo kwa njia ya Padri anamtolea Mungu Baba mwili na damu yake katika umbo la mkate na divai kama alivyojitolea mwenyewe juu ya msalaba… soma zaidi

a.gif Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa… soma zaidi

a.gif Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi rohoni anatenda dhambi gani?

Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi anatenda dhambi kubwa yaani kufuru Sakramenti.

26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. (1 Kor 11;26 - 27).. soma zaidi

a.gif Kampeni ya kutetea watoto yatima

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia kulea na kuwakuza watoto yatima kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto yatima kama walivyo watoto wengine nao ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae. Japokuwa hawana (wazazi) watu/mtu rasmi wa kuwatunza haimaanishi kuwa hawawezi kuwa watu wa maana baadae… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ni nini?

Ni Sakramenti ambayo Padri humuombea neema ya Mungu na kumpaka Mafuta Matakatifu mgonjwa aliye katika hatari ya kifo kwa ajili ya neema ya roho na mwili. (Yak 5:14-15, Mk 6:13).. soma zaidi

a.gif Walei wanaitwa na Mungu kufanya nini?

Walei wanaitwa na Mungu kuratibu malimwengu yote yafuate matakwa yake… soma zaidi

a.gif Komunyo pamba ndio nini?

Komunyo pamba ndio Ekaristi inayopokelewa na wale wanaokaribia kuaga maisha ya duniani na wanaojiandaa kuvukia uzima wa milele.. soma zaidi

a.gif Umwilisho maana yake ni nini?

Umwilisho ni ile hali ya Yesu kama Mungu kujifanya mtu kwa Bikira Maria mzaa. (Yoh 1:14).. soma zaidi

a.gif Amri kumi za Mungu ni zipi?

1. Ndimi Bwana, Mungu wako usiabudu miungu wengine.
2. Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
3. Fanya siku ya Mungu.. soma zaidi

a.gif Baada ya Mitume kufa ni nani wanafanya Sakramenti ya Ekaristi

Badaa ya Mitume kufa Maaskofu na Mapadri wanaendelea kuadhimisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.