MASOMO YA MISA, JUMANNE, JUNI 25, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Vyanzo vya sala za Kikristo


MASOMO YA MISA, JUMANNE, JUNI 25, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

SOMO 1

Mwa. 13 : 2, 5-18

Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha na kwa dhahabu. Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng’ombe na kondoo, na hema. Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja. Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi. Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu. Je! nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.

Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri hapo unapowenda Soari. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma. Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.

Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, na uzao wako nao utahesabika. Ondoka, ukatembee katika nchi hii, katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo. Basi Abramu akajongeza hema yake akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea Bwana madhabahu huko.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 15:1-5 (K) 1

(K) Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?

Bwana ni nani atakayekaa katika hema yako?
Ni mtu aendaye kwa ukamilifu na kutcnda haki
asemaye kweli kwa moyo wake. (K)

Asiyesingizia kwa ulimi wake,
Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa.
Bali huwaheshimu wamchao Bwana. (K)

Hakutoa fedha yake apatc kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele. (K)

SHANG1LIO

Zab. 119:105

Aleluya, aleluya,
Neno lako ni taa ya miguu yangu,
na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.

INJILI

Mt. 7:6,12-1

Yesu aliwaambia wanafunzi wake; Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeeni vivyo hivya hiyo” maana hiyo ndiyo torati na manabii. Ingieni kwa kupitia mlango uliyo mwembamba, maana, mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Injili ya Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Ni nani anayetoa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?

Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa hutolewa na kuhani tuu yaani Askofu au Padri.. soma zaidi

a.gif Kanisa kuwa moja maana yake nini?

Kanisa kuwa moja maana yake ni “mwili mmoja na Roho mmoja”: lina “Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Ef 4:4-5)… soma zaidi

a.gif Abramu Amwokoa Loti

1 Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu,.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMANNE, JUNI 25, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMANNE, JUNI 25, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE II

[Tafakari ya Sasa] 👉Siri ya Imani kwa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Ambrosi

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

a.gif Je, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia?

Ndiyo, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia, kwa sababu kwa njia yake tu tunatiwa uzima: sasa rohoni kwa kuondolewa dhambi, na siku ya mwisho mwilini pia kwa kufufuliwa… soma zaidi

a.gif Kutolea Misa kwa Marehemu maana yake ni nini?

Kutolea Misa kwa Marehemu ni kutolea Misa kwa ajili ya roho zilizoko toharani ili ziweze kuingia mbinguni.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Askofu anampiga kofi kidogo shavuni wakati akitoa Kipaimara?

Askofu anampiga kofi Kidogo Shavuni ili kumkumbusha awe mvumilivu, imara na tayari kuteseka hata kama ni kifo kwa ajili ya Yesu Kristo… soma zaidi

a.gif Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?

Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba Wayahudi walipokea watoto katika dini yao kwa kuwatahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa.

“Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu” (Lk 2:21)… soma zaidi

a.gif Mungu aliwaamuru nini watu wa kwanza?

Mungu aliwaamuru watu wa kwanza wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasije wakafa. (Mw 2:16-17).. soma zaidi

a.gif Je, ibada zetu ziishie katika kusadiki?

Hapana, ibada zetu zisiishie katika kusadiki, kwa kuwa tangu Agano la Kale Mungu aliagiza matendo mbalimbali ya ibada yanayolisha imani… soma zaidi

a.gif Mambo yanayomzuia mtu kuishi maisha mema ni yapi?

Mambo hayo ni;
1. Dhambi
2. Vilema
3. Vishawishi.. soma zaidi

a.gif Masifu ni nini?

Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu.. soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidi

a.gif Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?

Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha "Mungu Mtawala".. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.