MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 9, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Vyanzo vya sala za Kikristo

SOMO 1

Mwa. 32:23-33

Yakobo aliondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo.

Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusu panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda. Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.

Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi vangu imeokoka. Jua likamzukia akivuka Penueli, akachechemea kwa sababu ya paja la mguu wake. Kwa hiyo wana wa Israeli hawali ule mshipa ulio katika uvungu wa paja hata leo; maana alimgusa Yakobo panapo uvungu wa paja katika mshipa wa kiuno.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 17 :1-3, 6-8, 15 (K) 15

(K) Nikutazame uso wako katika haki..

Ee Bwana, usikie haki, ukisikilize kilio changu,
Utege sikio lako kwa maombi yangu,
Yasiyotoka katika midomo ya hila. (K)

Hukumu yangu na itoke kwako,
Macho yako na yatazame mambo ya adili.
Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,
Umenihakikisha usione neno;
Nimenuia kinywa changu kisikose. (K)

Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu.
Dhihirisha fadhili zako za ajabu,
Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;
Kwa mkono wako wa kuume
Uwaokoe nao wanaowaondokea. (K )

Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
mimi nikutazame uso wako katika haki,
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako. (K)

SHANGILIO

Yn. 10 : 27

Aleluya, aleluya,
Kondoo wangu waisikia sauti yangu,
nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.

INJILI

Mt. 9: 32-39

Walimletea Yesu mtu bubu mwenye pepo. Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wa kastaajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote. Lakini Mafarisayo wakisema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.

Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kondoo wasio na mchungaji. Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Neno la Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anatenda kazi zake?

Roho Mtakatifu anatenda kazi zake kwa njia hizi;
1. Anatuangaza kwa Mwanga wake tupate kuelewa mafundisho ya dini
2. Anatupatia neema za msaada za kutusaidia kutunza utakatifu wetu.. soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Vishawishi vinatokana na nini?

Vishawishi vinatokana na;
1. Shetani
2. Watu
3. Vitu.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 9, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 9, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nitaweka uadui

[Tafakari ya Sasa] 👉Uzuri wa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Anna

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

ufufuo-wa-wafu-upooo.JPG

a.gif Mafundisho ya kumfundisha mtu mzima kabla ya ubatizo wa hatari

Ni lazima asadiki kwamba;.. soma zaidi

a.gif Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Visakramenti

Haya ndiyo mambo yanayoulizwa sana kuhusu visakramenti.. soma zaidi

a.gif Rehema hutolewa na nani?

Rehema hutolewa na Kanisa Katoliki kwa kutugawia mastahili ya Yesu Kristo, Bikira Maria na Ya Watakatifu.. soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo.. soma zaidi

a.gif Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22).. soma zaidi

a.gif Ufukara wa kitawa ni nini?

Ufukara wa kitawa ni kutokuwa na mali Binafsi au kutotumia mali binafsi bila ruhusa. Ni kuitunza mali ya jamii kwa uangalifu na pia kuridhika na yale yapatikanayo. (Mt 19:16,21).. soma zaidi

a.gif Siku za Dominika Kanisa huadhimisha nini?

Kila Dominika Kanisa Huadhimisha kumbukumbu ya Fumbo la Pasaka; Yaani;.. soma zaidi

a.gif Nani ana lazima ya kufunga?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula. (Jumatano ya Majivu).. soma zaidi

a.gif Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?

Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.