MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 2, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 2, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

Somo la Kwanza

Mwa 19:15-29

Hata alfajiri ndipo malaika walimhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyohurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako; usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa.

Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waiiokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi. Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana, nave akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.

Wimbo wa katikati

Zab 26:2-3,9-12

Ee Bwana, unijaribu na kunipima;
Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.
Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,
Nami nimekwenda katika kweli yako.
(K) Fadhili zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.

Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,
Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.
Mikononi mwao mna madhara,
Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.
(K) Fadhili zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.

Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu;
Unikomboe, unifanyie fadhili.
Mguu wangu umesimama palipo sawa;
Katika makusanyiko nifamhimidi Bwana.
(K) Fadhili zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.

Shangilio

Yn 14:23

Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda, atalishika neno langu, na Baba yangu atampenda, na sisi tutakuja kwake.
Aleluya.

Somo la Injili

Mt 8:23-27

Yesu alipanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?


a.gif Mafundisho ya kumfundisha mtu mzima kabla ya ubatizo wa hatari

Ni lazima asadiki kwamba;.. soma zaidi

a.gif Lini Yesu aliacha maisha ya kijijini akaanza utume wake?

Yesu aliacha maisha ya kijijini akaanza utume wake miezi tu baada ya Yohane Mbatizaji, jamaa yake, kuwatikisa Wayahudi wote akihubiri wawe tayari kwa ujio wa mtu mkubwa zaidi, akisema,.. soma zaidi

a.gif Watoto wa Nuhu ni wepi?

Watoto wa Nuhu ni Shemu, Hamu na Nefteli.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 2, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 2, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉AMRI ZA MUNGU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Na ahimidiwe Bwana Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Picha ya Yesu wa Huruma

misaadas.gif

a.gif Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?

Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa… soma zaidi

a.gif Katika amri ya pili ya Mungu tumekatazwa nini?

Katika amri ya pili ya Mungu tunakatazwa kuapa bure kwa Jina la Mungu.. soma zaidi

a.gif Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali… soma zaidi

a.gif Mtakatifu Mathayo Mtume

Mathayo (kwa Kiebrania מַתִּתְיָהוּ, Mattityahu au מתי, Mattay, Zawadi ya Mungu; kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa hasa kutokana na Injili yenye jina lake. Labda aliitwa pia Lawi… soma zaidi

a.gif Nini maana ya Roho Mtakatifu?

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26).. soma zaidi

a.gif Mungu aliumba Malaika katika hali gani?

Mungu aliumba Malaika katika hali njema na heri kubwa… soma zaidi

a.gif Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?

Hapana, si mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote, bali mengine yanahitaji mhudumu wake awe amepewa daraja inayoshirikisha uwezo ambao Yesu aliwapa Mitume wake.

“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Lk 6:12-13)… soma zaidi

a.gif Mungu alinena na nani?

Alinena na;.. soma zaidi

a.gif Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu… soma zaidi

a.gif Sikukuu Kubwa Kupita zote Katika Kanisa ni ipi?

Sikukuu Kubwa Kupita zote Katika Kanisa ni PASAKA.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.