MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 16, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 16, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

SOMO 1

Kut. 2 :1-15

Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi aliondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.

Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta. Akaifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? Binti Farao akamwambia, Haya! enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonvesha. Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini.

Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga. Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake. Mbona unampiga mwenzako? Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! jambo lile limejulikana. Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 69 :3, 14, 30-31, 33-34 (K) 32

(K) Enyi mmtafutao Mungu,

mioyo yenu ihuishwe,
kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji.

Uniponye kwa kunitoa matopeni,
Wala usiniache nikazama
Na niponywe nao wanaonichukia,
Na katika vilindi vya maji. (K)

Wakanipa uchungu kuwa chakula changu;
Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
Meza yao mbele yao na iwe mtego;
Naam, wakiwa salama na iwe tanzi. (K)

Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
Nayo yatampendeza Bwana kuliko ng’ombe,
Au ndama mwenye pembe na kwato. (K)

Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafunga wake.
Mbingu na nchi zimsifu,
Bahari na vyote viendavyo ndani yake. (K)

SHANGILIO

Zab. 119:18

Aleluya, aleluya,
Unifumbue macho yangu niyatazame,
maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.

INJILI

Mt. 11 :20-24

Yesu alianza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

Nawe Kapernaumu, je! utakuzwa mpaka mbinguni? utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.

Neno la Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Tafakari: Je tunamkumbuka Mungu wakati gani?

Msimamizi wa ujenzi alikuwa anamwita mjenzi chini ya jengo yeye akiwa ghorofa ya 16. Lakini kwa sababu ya kelele za nje, mjenzi pale chini hakusikia sauti hiyo… soma zaidi

a.gif Ni ishara gani zinazoshuhudia ufufuko wa Yesu?

Ni ishara zifuatazo;.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa inaadhimishwaje?

Inaadhimishwa kwa Padre kumuombea mgonjwa, kumuwekea mikono na kumpaka mafuta katika panda la uso na viganja vya mikono; kwa kutumia mafuta aliyobariki Askofu siku ya Alhamisi kuu… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 16, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 16, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Majitoleo

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nipeleke Mbinguni Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa siku zote

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Karoli Lwanga

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

waliokufa-zaman-wapo-wap.JPG

a.gif Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti huenda wapi?

Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti hutupwa motoni milele. (Mt 25:41).. soma zaidi

a.gif Je magoti yanayopigwa wakati mwingine tofauti na wakati wa kuabudu yana maana gani?

Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwa Mkao wa sala.. soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Uzima wa milele

Maswali na majibu kuhusu uzima wa milele;.. soma zaidi

a.gif Habari njema kwa watu wote maana yake ni nini?

Maana yake ni;.. soma zaidi

a.gif Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu… soma zaidi

a.gif Mungu ametufunulia nini?

Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu… soma zaidi

a.gif Kanisa linatoa visakramenti kwa nani?

Kanisa linatoa visakramenti hata kwa waamini wenye vizuio na kwa wasio Wakristo, kwa sababu vinaeleweka na kuthaminiwa kwa urahisi, kwa kuwa zinasaidia kufurahia maisha… soma zaidi

a.gif Je, Biblia zote ni sawa?

Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza… soma zaidi

a.gif Makala mpya kwa sasa

Makala Mpya ni kama ifuatavyo,.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.