MASOMO YA MISA, JUMANNE, AGOSTI 6, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SIKUKUU YA KUNG’ARA BWANA WETU

SOMO 1

Dan 7: 9-10, 13-14

Mimi nilitazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.

Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu nave. Nave akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 97 : 1-2, 5-6, 9 (K) 1, 9

(K) Bwana ametamalaki, juu sana kuliko nchi yote.

Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa vingi na vifurahi.
Mawingu na giza vyamzunguka,
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. (K)

Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,
Mbele za Bwana wa dunia yote.
Mbingu zimetangaza haki yake,
Na watu wote wameuona utukufu wake. (K)

Maana Wewe, Bwana, ndiwe Uliye juu,
Juu sana kuliko nchi yote;
Umetukuka sana juu ya miungu yote. (K)

SOMO 2

2 Pet. 1:16-19

Hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.

Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

SHANGILIO

Mt 17: 5

Aleluya, aleluya,
Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu,
ninayependezwa naye, msikieni yeye.
Aleluya.

INJILI

Mt 17: 1-9

Yesu aliwatwaa Petro, na Yakobo, na Yohane nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye. Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana. Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msio- gope. Wakainua macho yao, wasione mtu ila Yesu peke yake.

Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Tupendane

Wapenzi tupendane,.. soma zaidi

a.gif Muamuzi wa Mwisho ni Mungu

Mungu ndiye Muamuzi;.. soma zaidi

a.gif Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?

Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMANNE, AGOSTI 6, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMANNE, AGOSTI 6, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA MBELE YA KITI CHA ENZI CHA MUNGU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kristu alijinyenyekesha

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwenye Huruma

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Maria Goretti

[Jarida La Bure] 👉NOVENA YA ROHO MTAKATIFU

misaadas.gif

a.gif Tupendane

Wapenzi tupendane,.. soma zaidi

a.gif Uvivu ni nini?

Uvivu ni uregevu wa moyo unaotufanya tukose juhudi.. soma zaidi

a.gif Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

Angalizo; Tunapoongelea kuhusu pombe sio kwamba tunahamasisha kutumia pombe bali tuelewe kile tunachofanya kwa mapenzi ya Mungu!
pombe haikukataliwa ila itumike kwa kiasi… soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Upendo Mkuu wa Mungu

Mungu alimpenda sana binadamu hata akauvaa Mwili wa Binadamu akashuka duniani na kuishi kama Binadamu ili amkomboe Mwanadamu na hata akaamua kufa kwa ajili ya Binadamu kwa malipizi ya dhambi za Binadamu na kwa maondoleo ya dhambi… soma zaidi

a.gif Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake… soma zaidi

a.gif Mtaguso Mkuu unasema nini kuhusu kusudi la maisha ya Utawa?

Kusudi la maisha ya Utawa ni;
1. Kutoa Ushuhuda wa Kristo na Kanisa na kutimiza mapenzi ya Mungu
2. Kujitoa kwa Kanisa ambapo kwa Jina la Mungu Kanisa linapokea Nadhiri za Mtawa, Linazilinda kwa Sheria yake, kuzilisha kwa Sakramenti na Mafundisho yake… soma zaidi

a.gif Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > “hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42)… soma zaidi

a.gif Biblia nzima ina vitabu vingapi?

Biblia nzima ina vitabu 73.. soma zaidi

a.gif Mafundisho ya dini kuhusu Marehemu

Kuhusu Marehemu;.. soma zaidi

a.gif Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?

Majina haya;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.