MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, SEPTEMBA 14, 2019 JUMA LA 23 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, SEPTEMBA 14, 2019 JUMA LA 23 LA MWAKA

SIKUKUU YA KUTUKUKA KWA MSALABA

SOMO 1

Hes. 21:4 – 9

Siku zile jangwani, watu walimnung’unikia Mungu, na Musa, mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, tumefanya dambi kwa sababu tumemnung’unukia Mungu, na wewe, utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi, Musa akawaombea watu. Bwana akawaambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo, ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 78:1 – 2, 34 – 38 (K) 7

(K) Msiyasahau matendo ya Mungu.

Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,
Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
Na nifunue kinywa changu kwa mithali,
Niyatamke mafumbo ya kale. (K)

Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta;
Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.
Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao,
Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wako. (K)

Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,
Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.
Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,
Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. (K)

Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema,
Husamehe uovu wala haangamizi.
Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake,
Wala haiwashi hasira yake yote. (K)

SOMO 2

Fil. 2:6 – 11

Yesu Kristo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama wanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mung alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Ee Kristu tunakuabudu na kukutukuza, kwa kuwa umeikomboa dunia kwa msalaba wako.
Aleluya.

INJILI

Yn. 3:13 – 17

Yesu alimwambia Nikodemo: Hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume.. soma zaidi

a.gif Kristo maana yake nini?

Kristo maana yake ni “Aliyepakwa mafuta” awe kiongozi wa taifa lake walivyotabiri manabii wa kale… soma zaidi

a.gif MTAKATIFU VICENT WA RELENI

Maisha ya Mtakatifu Vicent wa Releni kwa ufupi;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, SEPTEMBA 14, 2019 JUMA LA 23 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, SEPTEMBA 14, 2019 JUMA LA 23 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Kanuni ya imani

[Wimbo Mzuri PA.gif] Bwana ndiwe mwenye haki

[Tafakari ya Sasa] 👉Toba, msamaha na Baraka

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Fransisko wa Sales

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

misaadas.gif

a.gif Nyimbo za Kwaresma za Katoliki

Hizi hapa nyimbo nzuri za Kwaresima zitakazokusaidia uwe na Kwaresima nzuri ya Tafakari.. soma zaidi

a.gif Sakramenti zipi hutolewa mara moja tuu na kwa nini?

Sakramenti zinazotolewa mara moja tuu ni Ubatizo, Kipaimara na Daraja Takatifu… soma zaidi

a.gif Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;.. soma zaidi

a.gif Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu kwa sababu tunapaswa kutumia kwa utukufu wake vipawa alivyotujalia, kama vile vya kujenga, kupamba, kuchonga, kuchora na kucheza. Kwa njia hizo tutokeze na kukoleza imani yetu na ya wenzetu… soma zaidi

a.gif Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kufanya nini?

Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila ya mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua… soma zaidi

a.gif MIUJIZA NA MATOKEO YA MUNGU NA WATAKATIFU

Ingiza kichwa cha habari cha Muujiza au matokeo hapa chini kwenye kaboksi kisha bofya mbele yake.. soma zaidi

a.gif Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu… soma zaidi

a.gif Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22)… soma zaidi

a.gif Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani… soma zaidi

a.gif Mkatoliki anaabuduje?

Mkatoliki anaabudu kwa kupiga goti au magoti mawili na ni mbele ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu tuu hasa wakati wa kuingia na kutoka kanisani.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.