MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JUNI 29, 2019 JUMA LA 12 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Tueleweje Maandiko Matakatifu?

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JUNI 29, 2019 JUMA LA 12 LA MWAKA

SHEREHE YA WATAKATIFU PETRO NA PAULO, MITUME

SOMO 1

Mdo. 12:1-11

Herode mfalme alinyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohane, kwa upanga. Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa. Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.

Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa amelala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.

Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 34 :1-8 (K) 7

(K) Malaika wa Bwana awaokoa wamchao.

Nitamhimidi Bwana kila wakati,
sifa zake kinywani mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
wanyenyekevu wasikie wakafurahi. (K)

Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana akanijibu,
akaniponya na hofu zangu zote. (K)

Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
akamwokoa na taabu zake zote. (K)

Malaika wa Bwana hufanya kituo,
akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema,
heri mtu yule anayemtumaini. (K)

SOMO 2

2 Tim. 4 : 6-8, 17-18

Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe
kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Mt. 16:18

Aleluya, aleluya, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda. Aleluya.

INJILI

Mt. 16 :13-19

Yesu alienda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena u Yohane Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiye Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.


a.gif Dhambi za uchafu huleta hasara gani?

Huleta hasara hizi;.. soma zaidi

a.gif Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi mpaka lini?

Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria.
Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni… soma zaidi

a.gif Ni nanai ana kosa kumuabudu Mungu?

Anayekosa kumuabudu Mungu ni yule;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JUNI 29, 2019 JUMA LA 12 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JUNI 29, 2019 JUMA LA 12 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Maria Bikira

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala ni chimbuko la Fadhila

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Faustina Kowalska

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

KADI-PONGEZI-MZAZI.JPG

a.gif Sisi binadamu tukoje?

Sisi binadamu ni umoja wa mambo mawili: roho iliyoumbwa na Mungu moja kwa moja, na mwili ulioumbwa naye kwa njia ya wazazi… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Roho Mtakatifu

Maswali yanayopenda kuulizwa kuhusu Roho Mtakatifu yamejibiwa hivi;.. soma zaidi

a.gif Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni zipi?

Sababu nyingine za Biblia kutojitosheleza ni kwamba mambo mengi muhimu hayakuandikwa,.. soma zaidi

a.gif Hasira ni nini?

Hasira ni kukasirika bure kuonea na kulipiza kisasi.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya SA-SE-SI-SO-SU

:::::"SA"::::::
:::::::"SE"::::::
:::::::::"SI"::::::
::::::::::"SO"::::::
::::::::::::"SU"::::::.. soma zaidi

a.gif Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa… soma zaidi

a.gif Umwilisho maana yake ni nini?

Umwilisho ni ile hali ya Yesu kama Mungu kujifanya mtu kwa Bikira Maria mzaa. (Yoh 1:14).. soma zaidi

a.gif Baada ya kufufuka Yesu alifanya nini?

Alikaa siku 40 katika nchi akaonekana na watu wengi akawatimizia Mitume mafundisho na kuweka Kanisa lake (Mt 28:16-20).. soma zaidi

a.gif Maana ya baraka ni ipi?

Maana ya baraka ni kumsifu Mungu kwa yale aliyokwishatujalia na kumuomba azidi kutujalia kadiri ya mahitaji ya wahusika. Mara nyingi inatolewa na mtu mwenye daraja au mamlaka fulani… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Kipaimara ni nini?

Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.