MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 13, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

KUMBUKUMBU YA MT. BONAVENTURE, ASKOFU NA MWALIMU WA KANISA

SOMO 1

Mwa. 49: 29-33; 50 :15-25

Yakobo aliwaamuru wanawe: Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia. Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa bani Hethi.

Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake. Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; nave atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake, akasema, Mwambieni Yusufu hivi, Nakuomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.

Nduguze wakaenda tena, wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako. Yusufu akawaambia, Msiogope, je! mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha, na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.

Akakaa Yusufu katika Misri, yeye na nyumba ya babaye. Akaishi lusuru miaka mia na kumi. Yusufu akaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu; na wana wa Makiri, mwana wa Manase, walizaliwa magotini mwa Yusufu. Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha kutoka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo. Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akisema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 105 :1-4, 6-7 (K) 69 :32.

(K) Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.

Aleluya.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake,
Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote. (K)

Jisifuni kwa jina lake lakatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
Mtakeni Bwana na nguvu zake,
Utafuteni uso wake siku zote. (K)

Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo wateule wake.
Yeye Bwana, ndiye Mungu wetu,
duniani mwote mna hukumu zake. (K)

SHANGILIO

1 Pet. 1 :25

Aleluya, aleluya,
Neno la Bwana hudumu hata milele,
na neno hilo ni neno lile jema
lililohubiriwa kwenu. Aleluya.

INJILI

Mt. 10:24-33

Yesu aliwafundisha mitume wake: Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli; je! si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?

Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana. Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba. Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum. Je! mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu; lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi; bora nyinyi kuliko mashomoro wengi.

Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

Neno la Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Katika Amri ya kwanza ya Kanisa tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusikilize Misa kila siku ya Mungu na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidi

a.gif Ndoa ya utofauti wa Imani maana yake ni nini?

Ndoa ya utofauti wa Imani ni ndoa kati ya Mkristo Mkatoliki na mtu ambaye hajabatizwa kwa mfano Mpagani, Mwislamu, Yehova, Mlokole tangu kuzaliwa n.k.. soma zaidi

a.gif Loti na Binti Zake (Watoto wa Loti walivyozaa na Baba yao)

30 Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 13, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 13, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Tunakushukuru Mama Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Makusudi ya Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Brigita wa Sweeden

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

ni-halali-kwa-bikira-maria-kutuombes.JPG

a.gif Tafakari ya Zaburi 127:1-2

Leo tunatafakari Zaburi ya 127:1-2 kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Kuna Ubatizo wa namna ngapi?

Kuna Ubatizo wa namna tatu;
1. Ubatizo wa maji - Ubatizo wa kawaida
2. Ubatizo wa tamaa - Mfano mtu akifa akiwa na nia ya kubatizwa au akitamani kubatizwa
3. Ubatizo wa Damu - Mtu akiifia Imani japo hajabatizwa.. soma zaidi

a.gif Asili ya uhai wote ni nani?

Asili ya uhai wote ni Mwenyezi Mungu. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwa 1:1)… soma zaidi

a.gif Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?

Ndiyo, “ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” (Zab 116:15)… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Malaika

Mambo ya Msingi kujua kuhusu Malaika;.. soma zaidi

a.gif Mtaguso Mkuu unasema nini kuhusu kusudi la maisha ya Utawa?

Kusudi la maisha ya Utawa ni;
1. Kutoa Ushuhuda wa Kristo na Kanisa na kutimiza mapenzi ya Mungu
2. Kujitoa kwa Kanisa ambapo kwa Jina la Mungu Kanisa linapokea Nadhiri za Mtawa, Linazilinda kwa Sheria yake, kuzilisha kwa Sakramenti na Mafundisho yake… soma zaidi

a.gif Je, dhambi zote zinahusiana?

Ndiyo, dhambi zote zinahusiana kwa sababu dhambi zinazaa dhambi nyingine ndani mwetu na katika mazingira yetu… soma zaidi

a.gif Wazazi wa Bikira Maria ni nani?

Wazazi wa Bikira Maria ni Yoakimu na Anna.. soma zaidi

a.gif Ushauri wangu kwa leo, ni Heri kuchagua kunyamaza

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi

a.gif Ushirika wa watakatifu maana yake nini?

Ushirika wa watakatifu maana yake sisi, kwa kushiriki mafumbo matakatifu tunaunda ndani ya Kristo mwili mmoja, ambamo waadilifu waliopo duniani, marehemu wa toharani na wenye heri wa mbinguni tunaunganishwa na upendo tufaidike na mema ya kila mmoja… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.