MASOMO YA MISA, JULAI 7, 2019 DOMINIKA YA 14 YA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JULAI 7, 2019 DOMINIKA YA 14 YA MWAKA C

SOMO 1

Isa. 66:10 – 14

Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake. Maana Bwana asema hivi, Tazama, nitamwelekezea Amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu. Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa Bwana utajulikana, uwaelekeao watumishi wake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 66:1 – 7, 16, 20 (K) 1

(K) Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote.

Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
Imbeni utukufu wa jina lake.
Tukuzeni sifa zake,
Mwambieni Mungu, matendo yako yanatisha kama nini! (K)

Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,
Naam, italiimbia jina lako.
Njoni yatazameni matendo ya Mungu,
Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu. (K)

Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;
Katika mto walivuka kwa miguu;
Huko ndiko tulikomfurahia,
Atawala kwa uweza wake milele. (K)

Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu,
Name nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
Na ahimidiwe Mungu aliyeyakataa maombi yangu,
Wala kuniondolea fadhili zake. (K)

SOMO 2

Gal. 6:14 – 18

Mimi, hasha, nisione fahari juu ya kito chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, Amani na iwe kwao rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu. Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu. Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Yn. 1:12, 14

Aleluya, aleluya,
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.
Aleluya.

INJILI

Lk. 10:1 – 12, 17 – 20

Baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenye kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apelike watenda kazi katika mavuno yake. Enendeni, angalieni, nawatuma kama wanakondoo kati ya mbwa-mwitu. Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana wa Amani, Amani yenu itamkalia; la, hayumo, Amani yenu itarudi kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamehame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia. Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yenu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.
Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahaini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake… soma zaidi

a.gif Je kuna aina tofauti ya dhambi?

Ndiyo, kuna dhambi za mawazo, maneno, matendi na kutotimiza wajibu… soma zaidi

a.gif Neno la hekima la leo

HEKIMA YA LEO.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 7, 2019 DOMINIKA YA 14 YA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 7, 2019 DOMINIKA YA 14 YA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Tupokee Mama Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Mambo muhimu katika sala

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Agostino wa Hippo

mwili-utakaofufuliwa-ni-huu.JPG

a.gif Alipokwisha umba watu Mungu aliwafundisha nini?

Alipokwisha umba watu Mungu aliwafundisha Dini (Mwa 2:15-17).. soma zaidi

a.gif Je, tunaweza kuambatana na Yesu tukilikataa Kanisa?

Hapana, hatuwezi kuambatana na Yesu kwa kulikataa Kanisa, kwa kuwa hao wawili ni mwili mmoja, kama Bwanaarusi na Bibiarusi… soma zaidi

a.gif Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu ngapi?

Vitabu vya Agano Jipya Vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Injili (4)
2. Kitabu cha Matendo ya Mitume.. soma zaidi

a.gif Kwa namna gani Mungu Baba ndiye asili na lengo la Liturujia?

Mungu Baba ndiye asili na lengo la Liturujia kwa sababu katika liturujia anatujaza Baraka zake katika Mwanae Yesu Kristo, naye anatumiminia Roho Mtakatifu mioyoni mwetu.. soma zaidi

a.gif Kanisa ni la Kitume maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kitume maana yake wakubwa wake yaani Baba Mtakatifu na Maaskofu nimahalifa wa Mitume.. soma zaidi

a.gif Kisa cha Noa na Wanawe

18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani… soma zaidi

a.gif Kabla ya kuungama ni lazima kufanya nini?

Kabla ya kuungama ni lazima kukusudia kuacha dhambi na kuepuka nafasi kubwa ya dhambi bila kusahau kufuata hatua sita za kabla na baada ya kupokea kupokea Sakramenti ya Kutubio ambazo ni,.. soma zaidi

a.gif Yakobo Mkubwa

Yakobo, mwana wa Zebedayo na Salome, na kaka wa Mtume Yohane, alikuwa Myahudi wa karne ya 1 aliyepata kuwa mmoja kati ya Mitume wa Yesu muhimu zaidi… soma zaidi

a.gif Ubikira au Usafi kamili maana yake ni nini?

Ni kujinyima Ndoa kwa hiari na kutunza usafi wa Moyo kadiri ya Amri ya Sita na Tisa ya Mungu kwa maisha yote… soma zaidi

a.gif Mungu alimwumbaje Eva (Hawa)?

Mungu alimwumba Eva kwa mfupa wa ubavu kutoka kwa Adamu, akamtia roho. (Mwa 2:21-24).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.