MASOMO YA MISA, JULAI 28 2019: DOMINIKA YA 17 YA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JULAI 28 2019: DOMINIKA YA 17 YA MWAKA C

SOMO LA 1

Mwa 18:20-32

Bwana alisema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi. na dhambi zao zimeongezeka sana. basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hu- tauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Hasha, usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, Je! utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema. Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu. Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

WIMBO WA KATIKATI

Zab 138:1-3,6-9

Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
(K)Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umekuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita uliniitikiu,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
(K)Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu,
Naye amjua mwenyc kujivuna tokca mbali.
Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha,
Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu.
(K)Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
Bwana atanitimiliza mambo yangu;
Ec Bwana, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.
(K)Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

SOMO LA 2

Kol 2:12-14

Mkazikwa pamoja na Kristo katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yotc; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.

SHANGILIO

Yn 14:23

Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda, atashika neno langu, na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake.
Aleluya.

INJILI

Lk 11:1-13

Yesu alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni]. Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.] Utupe siku kwa siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie maiaribuni [lakini tuokoe na vule mwovu]. Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafifi yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa. nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake. Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?


a.gif Asili na matumizi ya Neno "AMINA" kama kiitikio muhimu katika Liturujia

Kiitikio hicho tunakifahamu sisi sote; tunaitikia mara nyingi lakini je, tunaelewa umuhimu wake? Binafsi nikichunguza wakati wa maadhimisho mbalimbali ya Liturujia hasa Adhimisho la Ekaristi, ni baadhi tu ya waamini wanaoitikiaAmina sehemu mbalimbali wakati wa Misa. Waamini wengine huitikia  kwa sauti  ya kuungama dhambi na wengine hawaitikii kabisa… soma zaidi

a.gif Mambo ya kufahamu katika kipindi cha kwaresima

Kwa kipindi cha Kwaresma haya ndiyo mambo muhimu unayopaswa kuyajua… soma zaidi

a.gif Zifahamu dhambi ambazo huondolewa na PAPA pekee au Padre kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu

ZIFAHAMU DHAMBI AMBAZO HUONDOLEWA NA PAPA PEKEE AU PADRE KWA MAMLAKA MAALUMU KUTOKA KWA PAPA :.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 28 2019: DOMINIKA YA 17 YA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 28 2019: DOMINIKA YA 17 YA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA MTAKATIFU INYASI

[Wimbo Mzuri PA.gif] Neema ya Roho Mtakatifu

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Fransisko wa Sales

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

KADI-MMISI-MZAZI.JPG

a.gif Padri anaondolea dhambi mahali pa nani?

Padri anaondolea dhambi mahali pa Mungu.. soma zaidi

a.gif Lengo la mali ya binafsi ni lipi?

Kutosheleza mahitaji yake mtu binafsi, ya familia, ya wenye shida na ya kanisa… soma zaidi

a.gif Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu maana yake ni nini?

Tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu maana yake tuna roho zenye akili na utashi yaani uwezo wa kutofautisha mema namabaya, na zitakazoishi milele… soma zaidi

a.gif Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Malaika

Mambo ya Msingi kujua kuhusu Malaika;.. soma zaidi

a.gif Mashauri ya Injili ni nini?

Ni mwaliko wa kuchagua kwa hiari kuishi;
1. Ufukara
2. Utii
3. Ubikira au usafi kamili kwa ajili ya ufalme wa Mungu (Mk 10:29-30).. soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

a.gif Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu? Na kwa nini aheshimiwe?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu kwa sababu amemzaa Yesu na Yesu ni Mungusoma zaidi

a.gif Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13).. soma zaidi

a.gif Katika Amri ya Kwanza ya kanisa tumekatazwa nini?

Tumekatazwa;
1. Kukosa Misa
2. Kufanya kazi nzito siku hizo.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.