MASOMO YA MISA, JULAI 27, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 16 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Kut. 24:3-8

Musa aliwambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda. Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng’ombe.
Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 50:1-2, 5-6, 14-15 (K) 14

(K) Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru.

Mungu, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi,
Toka maawio ya jua hata machweo yake.
Tokea Sayuni,, ukamilifu wa uzuri,
Mungu amemulika. (K)

Nikusanyieni wacha Mungu wangu,
Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Na mbingu zitatangaza haki yake,
Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu. (K)

Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;
Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
Ukaniite siku ya mateso;
Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. (K)

SHANGILIO

Zab. 8:15

Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.

INJILI

Mt. 13:24 – 30

Yesu aliwatolea makutano mfano akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala akaja adui yake akapanda magugu katikati ya agano, akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Rehema ni nini?

Rehema ni msamaha au ondoleo la adhabu ya dhambi tulizostahili sababu ya dhambi zilizokwisha ondolewa.. soma zaidi

a.gif Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?

Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake mafumbo hayakuadhimishwa vizuri… soma zaidi

a.gif Mambo muhimu kujua kuhusu Ubatizo

Haya hapa maswali na majibu kuhusu maswala ya Ubatizo;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 27, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 16 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 27, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 16 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Kuweka nia njema

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni Mwaminifu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Gemma Galgani

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG

a.gif Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;.. soma zaidi

a.gif Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;.. soma zaidi

a.gif Kuna Rehema za namna ngapi?

Rehema za namna mbili.. soma zaidi

a.gif Litania ya Huruma ya Mungu

Litania ya Huruma ya
Mungu.. soma zaidi

a.gif Amani ya Moyoni au Rohoni

Amani ya Moyoni au Rohoni ni hali ya kutokua na wasiwasi na hofu moyoni kuhusu Mambo ya Rohoni na ya kidunia… soma zaidi

a.gif Papa amejaliwa na Mungu mamlaka gani?

Papa amejaliwa na Mungu mamlaka kamili juu ya waamini wote awafungulie ufalme wa mbinguni, kama Yesu alivyomuambia Petro: “Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Math 16:19)... soma zaidi

a.gif Loti na Binti Zake (Watoto wa Loti walivyozaa na Baba yao)

30 Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili… soma zaidi

a.gif Mkristo Hupokea Sakramenti ya Kipaimara Mara ngapi?

Mkristo Hupokea Sakramenti ya Kipaimara Mara moja tuu, kwa sababu Kipaimara hupiga rohoni chapa isiyofutika milele… soma zaidi

a.gif Kwa njia ya watawa Kanisa linaonyesha nini mbele ya watu wote?

Kanisa linaonyesha jinsi Yesu alivyotenda mahali popote pale alipopita kwa mfano wagonjwa, maskini, wakosefu, watoto, vilema, wenye njaa na wasiojua habari njema.. soma zaidi

a.gif Maana ya sanamu ndani ya Kanisa Katoliki

Haya ndiyo majibu ya Maswali yote yanayoulizwa kuhusu Sanamu Kanisani.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.