MASOMO YA MISA, JULAI 24, 2019: JUMATANO, JUMA LA 16 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JULAI 24, 2019: JUMATANO, JUMA LA 16 LA MWAKA

SOMO 1

Kut. 16:1-5, 9-15

Walisafiri kutoka Elimu, na mkutano wote wa wana wa Israeli wakafikilia bara ya Sini, iliyoko kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri. Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani; wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa Bwana katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.
Ndipo Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo. Kisha itakuwa siku ya sita, ya kwamba watayaandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa ni mara mbili kuliko wayaokotayo kila siku.
Musa akamwambia Haruni, Haya, sema na mkutano wote wa wana wa Israeli. Njoni karibu mbele ya Bwana; kwa kuwa yeye ameyasikia manung’uniko yetu. Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa Bwna ukaonekana katika hilo wingu. Bwana akasema na Musa, akinena, Nimeyasikia manung’uniko ya wana wa Israeli; haya! Sema nao, ukinena, Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Ikawa wakati wa jioni; kware wakakaribia, wakakifunikiza kituo; na wakati wa asubuhi umande ulikuwa juu ya nchi pande zote za kituo. Na ulipoinuka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama sakitu juu ya nchi.
Wana wa Israeli walipokiona, wakaambiana, Nini hiki? Maana hawakujua ni kitu gani. Musa akawaambia, Ndio mkate ambao Bwana amewapa ninyi, mle.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 78:18-19, 23-28 (K) 24

(K) Bwana aliwapa nafaka ya mbinguni.

Wakamjaribu Mungu mioyoni mwao
Kwa kutaka chakula kwa tamaa zao.
Naam, walimwambia Mungu, wakasema,
Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani? (K)

Lakini aliyaamuru mawingu juu;
Akaifungua milango ya mbinguni;
Akawanyeshea mana ili wale;
Akawapa nafaka ya mbinguni. (K)

Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;
Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.
Aliuelekeza upepo wa mashariki mbinguni;
Akaiongoza kusi kwa uweza wake. (K)

Akawanyeshea nyama kama mavumbi,
Na ndege wenye mbawa,
Kama mchanga wa bahari.
Akawaangusha kati ya matuo yao,
Pande zote za maskani zao. (K)

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Mbegu ni neno la Mungu, anayepanda ni Kristu, atakayemkuta, ataishi milele.
Aleluya.

INJILI

Mt. 13:1 – 9

Yesu alitoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. Mwenye masikio na asikie.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Kwa kugusa mabega tuna maana gani?

Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote.. soma zaidi

a.gif Anayebatizwa yampasa nini?

Yampasa kuungama imani yake ama mwenyewe akiwa mtu mzima ama kupitia wazazi kama akiwa mtoto mdogo.. soma zaidi

a.gif Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine?

Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Yosefu likufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni “Bikira daima”… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 24, 2019: JUMATANO, JUMA LA 16 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 24, 2019: JUMATANO, JUMA LA 16 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA MAMA WA MATESO

[Wimbo Mzuri PA.gif] Ewe Mama Uliyeumbwa

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwenye haki

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu John Bosco

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

BIKIRA-MARIA-KUITWA-MAMA-WA-MUNGU-KWA-NINI.JPG

a.gif Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10).. soma zaidi

a.gif Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi

Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi ni kama Ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Zifahamu dhambi ambazo huondolewa na PAPA pekee au Padre kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu

ZIFAHAMU DHAMBI AMBAZO HUONDOLEWA NA PAPA PEKEE AU PADRE KWA MAMLAKA MAALUMU KUTOKA KWA PAPA :.. soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidi

a.gif Uzima wa milele ni nini?

Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho… soma zaidi

a.gif Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga.. soma zaidi

a.gif Uzima wa milele

Maswali na majibu kuhusu uzima wa milele;.. soma zaidi

a.gif Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya nani?

Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya Yesu na Kanisa lake… soma zaidi

a.gif Ibada ya Daraja inachapa alama gani nafsini mwa aliyepewa?

1. Ibada ya Daraja inatia rohoni alama isiyofutika.. soma zaidi

a.gif Ni nani wahudumu wa Sakramenti ya ndoa?

Wahiudumu rasmi wa Sakramenti ya ndoa ni wachumba wenyewe, Padri kama shahidi rasmi wa kanisa. Tena ni lazima ifungwe mbele ya mashahidi wengine wawili… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.