MASOMO YA MISA, JULAI 23, 2019: JUMANNE , JUMA LA 16 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Kut. 14:21-15:1

Musa alinyosha mkono wake juu ya bahari; Bwana akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mono wa kuume, na mkono wa kushoto.
Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, Bwana akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa Bwana anawapigania, kinyume cha Wamisri.
Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkoon wake juu ya bahari, na kulippambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni makuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.
Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa. Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi wake.
Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 15:8-10, 12, 17 (K) 1

(K) Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana..

Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,
Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,
Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.
Adui akasema Nitafuatia, nitapata nitagawanya nyara,
Nafsi yangu itashibishwa na wao;
Nitaufuta upanga wangu,
Mkono wangu utawaangamiza. (K)

Ulinyosha mkono wako wa kuume,
Nchi ikawameza.
Ulivuma kwa upepo wako, bahari ikawafunikiza;
Wakazama kama risasi ndani ya maji makuu. (K)

Utawaingiza, na kuwapanda
Katika mlima wa urithi wako,
Mahali pale ulipojifanyia, Ee Bwana, ili upakae,
Pale patakatifu ulipopaweka imara, Bwana,
Kwa mikono yako. (K)

SHANGILIO

Zab. 130:5

Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

INJILI

Mt. 12:46 – 50

Yesu alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao… soma zaidi

a.gif Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10).. soma zaidi

a.gif Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kufanya nini?

Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kuishi kwa useja kama Yesu na Paulo, au kwa ndoa:.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 23, 2019: JUMANNE , JUMA LA 16 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 23, 2019: JUMANNE , JUMA LA 16 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo na chuki havitangamani

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG

a.gif Mtume Filipo

Filipo (kwa Kigiriki Φίλιππος, Philippos) ni jina la mfuasi wa Yesu Kristo anayeshika nafasi ya tano katika orodha zote nne za Mitume wa Yesu katika Agano Jipya… soma zaidi

a.gif Sherehe na tarehe ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo

by Fr TITUS AMIGU.. soma zaidi

a.gif Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu… soma zaidi

a.gif Je, Maria amechangia wokovu wetu?

Ndiyo, Maria amechangia wokovu wetu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa… soma zaidi

a.gif Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?

Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani… soma zaidi

a.gif Je, nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo?

Ndiyo, nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo, lakini ni vigumu zaidi, kwa sababu hatupati msaada wa sakramenti hiyo maalumu… soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidi

a.gif Kilichowapata Watu 8 waliowahi kumdhihaki Mungu

HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA… soma zaidi

a.gif Neno "Amina" katika sala lina maana gani?

Neno "Amina" katika sala lina maanisha "Na iwe Hivyo" (Hesabu 5:22).. soma zaidi

a.gif Ulafi ni nini?

Ulafi ni kupenda kula au kunywa bila kiasi.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.