MASOMO YA MISA, JULAI 21 2019: DOMINIKA YA 16 YA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JULAI 21 2019: DOMINIKA YA 16 YA MWAKA C

SOMO 1

Mwa. 18 : l-10

Bwana alimtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng’ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala. Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati uu huu mwakani. na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 15 (K) 1

(K) Bwana, ni nani atakayekaa katika hema yako

Bwana, ni nani atakayefanya maskani yake
Katika kilima chako kitakatifu?
Ni yeye aendaye kwa ukamilifu,
Na kutenda haki;
Asemaye kweli kwa moyo wake,
Asiyesingizia kwa ulimi wake. (K)

Yeye ambaye hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,
Bali huwaheshimu wamchao Bwana. (K)

Yeye ambaye hakutoa fedha yake apate kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele. (K)

SOMO 2

Kol 1 :24-28

Nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake, ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu; tumaini la utukufu; ambaye sisi tunamhubiri habari zake, tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

SHANGILIO

Yn. 14 :23

Aleluya, aleluya, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; Na Baba yangu atampenda; Nasi tutakuja kwake. Aleluya.

INJILI

Lk. 10 :38-42

Ikawa katika kuenenda kwao Yesu aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Kwa kuwa tumekombolewa kwa damu azizi ya Mwana wa Mungu, tunaonywa vipi?

Kwa kuwa tumekombolewa kwa damu azizi ya Mwana wa Mungu, tunaonywa kwamba,.. soma zaidi

a.gif IBADA YA HURUMA KUU YA MUNGU

Habari njema ni kwamba Yesu sasa anakuja kwako Kama Bwana wa Huruma, Mwalimu na Rafiki Mwema Akupendaye, Angalia Usichelewe Wakati akija Kama Hakimu asikukute bado huna ushirika nae na hujui haki na hukumu yake. Wakati ndo huu wa kukimbilia Huruma na Upendo wake wa Bure Kwako... soma zaidi

a.gif Kanisa kuwa la Mitume maana yake nini?

Kanisa kuwa la Mitume maana yake limejengwa juu ya Mitume 12 wa Yesu na kuongozwa na waandamizi wao… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 21 2019: DOMINIKA YA 16 YA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 21 2019: DOMINIKA YA 16 YA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Majitoleo

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nipeleke Mbinguni Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Toba, msamaha na Baraka

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Karoli Lwanga

KWA-NINI-TUNAMUHESHIM-MARIA.JPG

a.gif Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti huenda wapi?

Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti hutupwa motoni milele. (Mt 25:41).. soma zaidi

a.gif Je magoti yanayopigwa wakati mwingine tofauti na wakati wa kuabudu yana maana gani?

Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwa Mkao wa sala.. soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Uzima wa milele

Maswali na majibu kuhusu uzima wa milele;.. soma zaidi

a.gif Habari njema kwa watu wote maana yake ni nini?

Maana yake ni;.. soma zaidi

a.gif Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu… soma zaidi

a.gif Mungu ametufunulia nini?

Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu… soma zaidi

a.gif Kanisa linatoa visakramenti kwa nani?

Kanisa linatoa visakramenti hata kwa waamini wenye vizuio na kwa wasio Wakristo, kwa sababu vinaeleweka na kuthaminiwa kwa urahisi, kwa kuwa zinasaidia kufurahia maisha… soma zaidi

a.gif Je, Biblia zote ni sawa?

Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza… soma zaidi

a.gif Makala mpya kwa sasa

Makala Mpya ni kama ifuatavyo,.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.