MASOMO YA MISA, JULAI 14, 2019: DOMINIKA YA 15 YA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Kumb. 30:10 – 14

Ukiwa utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati; ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote. Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali. Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme. Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 68:13, 16, 29 – 30, 32 – 33, 35 – 36 (K) 32

(K) Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.

Nami maombi yangu nakuomba Wewe Bwana,
Wakati ukupendezao; Ee Mungu.
Kwa wingi wa fadhili zako unijibu.
Katika kweli ya wokovu wako.
Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema,
Kwa kadiri ya rehema zako unielekee. (K)

Nami niliye maskini na mtu wa huzuni.
Mungu, wokovu wako utaniinua.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani. (K)

Walioonewa watakapoona watafurahi;
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji.
Wala hawadharau wafunga wake. (K)

Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda,
Wazao wa watumishi wake watairithi,
Nao walipendao jina lake watakaa humo. (K)

SOMO 2

Kol. 1:15 – 20

Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake, akiisha kufanya Amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Mdo. 16: 14

Aleluya, aleluya!
Fungua moyo wetu, Ee Bwana, ili tuyatunze maneno ya Mwanao.
Aleluya.

INJILI

Lk. 10: 25 – 37

Siku ile, mwanasheria mmoja alisimama amjaribu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyanyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipitia kando. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapitia kando. Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake, yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Kilindi cha Huruma ya Mungu

Habari njema ni kwamba Yesu sasa anakuja kwako Kama Bwana wa Huruma, Mwalimu na Rafiki Mwema Akupendaye, Angalia Usichelewe Wakati akija Kama Hakimu asikukute bado huna ushirika nae na hujui haki na hukumu yake. Wakati ndo huu wa kukimbilia Huruma na Upendo wake wa Bure Kwako... soma zaidi

a.gif Ni kwa nini Sadaka ya Misa Takatifu ni Sadaka ile ile ya Msalaba?

Sadaka ya Misa Takatifu ni ile ile ya Msalaba kwa sababu ni sadaka moja tu, kuhani na kafara ni yule yule… soma zaidi

a.gif Neema ya Utakaso yapoteaje?

Neema ya Utakaso yapotea kwa kutenda dhambi kubwa (dhambi ya mauti).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JULAI 14, 2019: DOMINIKA YA 15 YA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JULAI 14, 2019: DOMINIKA YA 15 YA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Umepokewa kwa Shangwe

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Gemma Galgani

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

JE-MARIA-NI-MAMA-YETU-PIA.JPG

a.gif MIUJIZA NA MATOKEO YA MUNGU NA WATAKATIFU

Makala za Miujiza… soma zaidi

a.gif Njia Kuu 3 za Kuiishi Huruma ya Mungu

Kuna njia Tatu kuu za Kuiishi Huruma ya Mungu ambazo ni kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Ni nani aweza kupokea Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?

Ni kila Mkatoliki aliyefikia umri wa kufikiri na aliye katika hatari ya kufa kwa ugonjwa au uzee aweza kupokea Sakramenti hii… soma zaidi

a.gif Mtu ni nani?

Mtu ni kiumbe chenye mwili na roho kilichoumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. (Mwa 1:26).. soma zaidi

a.gif Je, Biblia zote ni sawa?

Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza… soma zaidi

a.gif Sherehe na tarehe ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo

by Fr TITUS AMIGU.. soma zaidi

a.gif Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?

Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake… soma zaidi

a.gif Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?

Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa kwa kuwa ndivyo anavyotufanya “tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo… tupate kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:4,12)… soma zaidi

a.gif Hatua za maisha ya kitawa ni zipi?

Hatua za maisha ya kitawa ni
1. Uaspiranti - Mtarajiwa wa Maisha ya Kitawa
2. Ukandidati - Mtarajiwa wa maisha ya kitawa
3. Upostulanti - uombaji wa Maisha ya kitawa.. soma zaidi

a.gif Mafundisho kuhusu kitubio

Maswali ya msingi kuhusu Kitubio;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.