MASOMO YA MISA, IJUMAA, JUNI 28, 2019: SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU KRISTO

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, IJUMAA, JUNI 28, 2019: SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU KRISTO

Somo la Kwanza

Eze 34:11-16

Bwana Mungu asema hivi: Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo zangu, na kuwaulizia. Kama vile mchungaji atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami nitawaokoa katika mahali yote walipotawanyika, katika siku ya mawingu na giza. Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu. Nami nitawalisha malisho mema, na juu ya milima ya mahali yalipoinuka pa Israeli litakuwa zizi lao; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli. Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana Mungu. Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu.

Wimbo wa katikati

Zab 23

Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu;
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
(K) Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.

Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza
Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
(K) Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.

Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.
(K) Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.

Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
(K) Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.

Somo la Pili

Rum 5:5-11

Pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Basi Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.

Shangilio

Yn 10: 14

Aleluya, aleluya.
Mimi ndimi mchungaji mwema;asema Bwana; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
Aleluya.

Somo la Injili

Lk 15: 3-7

Aliwaambia mfano huu, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aenda akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani yake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.


a.gif Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni nini?

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu.. soma zaidi

a.gif Mtume Bartolomayo

Bartolomayo (kwa Kigiriki Βαρθολομαιος) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu kadiri ya Injili Ndugu… soma zaidi

a.gif Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?

NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, IJUMAA, JUNI 28, 2019: SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU KRISTO

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, IJUMAA, JUNI 28, 2019: SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU KRISTO

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kristu amekuwa mtii

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa Mungu hauna mwisho

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

MUNGU-NI-MUNGU-BIKIRA-MARIA-ATAKUAJE-MAMA.JPG

a.gif Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

MKASA WA KUSISIMUA : MUNGU AKIPANGA KUKUINUA HAMNA ATAEWEZA KUZUIA, HATA SHETANI HATOWEZA… soma zaidi

a.gif Kuumbwa kwa mtu, Mungu alivyoumba binadamu

Mtu ni kiumbe pekee chenye mwili na roho kilichoumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Mungu alipotaka kumuumba mtu alisema "Tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu" (Mwa. 1:26-27).. soma zaidi

a.gif Kanisa linatoa ushahuri gani kuhusu ndoa halali au ya mseto?

Kanisa linatambua hatari kubwa kwa Imani linashauri watoto wake wawe na busara kubwa wanapoamua kupendana kwa lengo la kufunga ndoa… soma zaidi

a.gif Tujifunze kitu hapa

Siku moja mwanamke alitoka nje ya nyumba na kuwaona wazee watatu wenye mvi kichwani wakiwa wamekaa nje ya nyumba yake.
Hakuwatambua na wala hakuwa anawafahamu… soma zaidi

a.gif Kifungu cha Biblia kinachothibitisha kua Bikira Maria Mama wa Yesu ni Mama wa Wakristu Wote

Kwa ufupi.. soma zaidi

a.gif Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya nani?

Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya Yesu na Kanisa lake… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Neema na Rehema

Mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu Neema na Rehema.. soma zaidi

a.gif Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?

Maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo kwa sababu yanafafanua ishara nyingine na kuzitia nguvu ya kututakasa… soma zaidi

a.gif Biblia ina sehemu kuu ngapi?

Biblia ina sehemu kuu 2 (mbili) ambazo ni.. soma zaidi

a.gif Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake nini?

Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake ni kwamba, kabla hajazaliwa kama mtu duniani ni Mungu, sawa na Baba anayemzaa yeye tu tangu milele… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.