MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 5, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Mwa. 23:1-4, 19; 24:1-8, 62-67

Umri wake Sara ulikuwa miaka mia na ishirini na saba, ndio umri wake Sara. Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Ibrahimu akaja kumlilia Sara na kumwombolezea. Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake, akasema na bani Hethi, akinena, Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.

Basi baada ya hayo Ibrahimu akamzika Sara mkewe katika pango ya shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.

Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na Bwana alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote. Ibrahimu akamwambia mtumishi wake, mzee wa nyumba yake, aliyetawala vitu vyake vyote, Tafadhali uutie mkono wako chini ya paja langu, nami nitakuapisha kwa Bwana, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao; bali enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke. Yule mtumishi akamwambia, Labda yule mwanamke hatakubali kufuatana nami mpaka nchi hii, Ibrahimu akamwambia, Ujihadhari, usimrudishe mwanangu huko. Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babaangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake mbele yako, anwe utamtwalia mwanangu mke tokea huko; na yule mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi, utafunguliwa kiapo changu hiki; lakini usimrudishe mwanangu huko.

Basi isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana laikaa katika nchi ya kusini. Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja. Rebeka akainua macho, anaye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia. Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika. Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyoyatenda. Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamaake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 106:1-5 (K) 1

(K) Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema.

Aleluya.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,
kwa maana fadhili zake ni za milele.
Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya Bwana,
kuzihubiri sifa zake zote. (K)

Heri washikao hukumu,
Na kutenda haki sikuzote.
Ee Bwana, unikumbuke mimi,
Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. (K)

Unijilie kwa wokovu wako,
Ili niuone wema wa wateule wako.
Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako,
Na kujisifu pamoja na watu wako. (K)

SHANGILIO

Zab. 130:5

Aleluya, aleluya,
Roho yangu inamngoja Bwana,
na Neno lake nimelitumainia.
Aleluya.

INJILI

Mt. 9:9 – 13

Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.

Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Neno la Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Mungu ni nani?

Mungu ndiye muumba wa kila kitu katika uwingu na nchi, Mkubwa wa ulimwengu mwenye kuwatuza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya… soma zaidi

a.gif Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni nani?

Wazazi wa Yohani Mbatizaji ni Zakaria na Eizabeti.. soma zaidi

a.gif Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 5, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 5, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa wenye kuzimia

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Fransisko wa Sales

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

MUNGU-NI-MUNGU-BIKIRA-MARIA-ATAKUAJE-MAMA.JPG

a.gif Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;.. soma zaidi

a.gif Bikira Maria ni nani? Mambo makuu ya kushangaza usiyoyajua kuhusu Bikira Maria

Mpendwa msomaji, mara nyingi umekuwa ukijiuliza mengi kuhusu Bikira Maria. Leo nimekukusanyia maswali na majibu kuhusu mambo muhimu ambayo ungependa kuyajua kuhusu Bikira Maria kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani?

Yesu aliteswa hadi kuuawa msalabani ili abebe kwa upendo na kufidia dhambi za watu wote, alivyotabiriwa:.. soma zaidi

a.gif NI KWELI WAKATOLIKI WANAABUDU SANAMU ?

Kati ya dhambi ambazo kwa wakatoliki ndiyo wazi kwa watu ni dhambi ya kuabudu sanamu. Dhambi hii imewafanya wakatoliki waonekane au hawasomi Biblia au wanasoma ila hawaelewi au wanasoma na kuelewa lakini wamekuwa wakipuuza maandiko Matakatifu. Ubayana wa dhambi hii kwa wakatoliki ni kile wanachokifanya siku ya Ijumaa Kuu na mambo yanayoonekana katika nyumba za kuabudia kama makanisa ambapo sanamu lukuki zinaonekana, toka zile za vitu vya duniani hadi vile za mbinguni… soma zaidi

a.gif Je, divai (pombe) ni halali?

Ndiyo, divai ni halali, mradi itumike kwa kiasi isije ikaleta madhara… soma zaidi

a.gif Sakramenti za wazima ni zipi?

Sakramenti za wazima ni: Ekaristi Takatifu, Kipaimara, Mpako Mtakatifu, Daraja na Ndoa… soma zaidi

a.gif Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?

NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidi

a.gif Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo… soma zaidi

a.gif Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?

Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi.. soma zaidi

a.gif Je, wenye daraja wanastahili heshima?

Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.