MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 26, 2017 JUMA LA 16 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

KUMBUKUMBU YA WAT. YOAKIM NA ANNA, WAZAZI WA BIKIRA MARIA

SOMO 1

Ybs. 44:1, 10 – 15

Haya na tuwasifu watu wa utauwa, Na baba zetu katika vizazi vyao. Lakini hawa walikuwa watu wa utauwa, wala kazi zao za haki hazisahauliki. Wema wao utawadumia wazao wao, Na urithi wao una wana wa wana;

Wazao wao wanashikamana na agano, Na watoto wao kwa ajili yao. Kumbukumbu lao litadumu milele, Wala haki yao haifutiki kamwe; Miili yao imezikwa katika amani, Na jina lao laishi hata vizazi vyote. Mkutano wa watu wataitangaza hekima yao, Na makusanyiko watazihubiri sifa zao.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 132:11, 13 – 14, 17 – 18

(K) Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.

Bwana amemwapia Daudi neno la kweli,
Hatarudi nyuma akalihalifu,
Baadhi ya wazao wa mwili wako
Nitawaweka katika kiti chako cha enzi. (K)

Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni,
Ameitamani akae ndani yake.
Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele,
Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani. (K)

Hapo nitamchipushia Daudi pembe,
Na taa nimemtengenezea masihi wangu.
Adui zake nitawavika aibu,
Bali juu yake taji yake itasitawi. (K)

SHANGILIO

Lk. 2:15

Aleluya, aleluya,
Waliitarajia faraja ya Israeli,
na Roho Mtakatifu alikuwa juu yao.
Aleluya.

INJILI

Mt. 13:16 – 17

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao… soma zaidi

a.gif Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10).. soma zaidi

a.gif Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kufanya nini?

Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kuishi kwa useja kama Yesu na Paulo, au kwa ndoa:.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 26, 2017 JUMA LA 16 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 26, 2017 JUMA LA 16 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo na chuki havitangamani

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG

a.gif Mtume Filipo

Filipo (kwa Kigiriki Φίλιππος, Philippos) ni jina la mfuasi wa Yesu Kristo anayeshika nafasi ya tano katika orodha zote nne za Mitume wa Yesu katika Agano Jipya… soma zaidi

a.gif Sherehe na tarehe ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo

by Fr TITUS AMIGU.. soma zaidi

a.gif Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu… soma zaidi

a.gif Je, Maria amechangia wokovu wetu?

Ndiyo, Maria amechangia wokovu wetu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa… soma zaidi

a.gif Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?

Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani… soma zaidi

a.gif Je, nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo?

Ndiyo, nje ya kitubio tunaweza kuondolewa dhambi tuliyotenda baada ya ubatizo, lakini ni vigumu zaidi, kwa sababu hatupati msaada wa sakramenti hiyo maalumu… soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidi

a.gif Kilichowapata Watu 8 waliowahi kumdhihaki Mungu

HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA… soma zaidi

a.gif Neno "Amina" katika sala lina maana gani?

Neno "Amina" katika sala lina maanisha "Na iwe Hivyo" (Hesabu 5:22).. soma zaidi

a.gif Ulafi ni nini?

Ulafi ni kupenda kula au kunywa bila kiasi.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.