MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 19, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Kut. 11:10-12:14

Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.

Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwanakondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwanakondoo kwa watu wa nyumba moja; na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwanakondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwanakondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwanakondoo. Mwanakondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.

Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kutia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. Msiile mbichi wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.

Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.

Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 116:12-13, 15-18 (K) 13

(K) nitakipokea kikombe cha wokovu,

na kulitangaza jina la Bwana.

Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)

Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake.
Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Umevifunga vifungo vyangu. (K)

Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana;
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote. (K)

SHANGILIO

Zab. 119:28, 33

Aleluya, aleluya,
Unitie nguvu sawasawa na neno lako,
ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.

INJILI

Mt. 12:1 – 8

Wakati ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.

Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao? Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia? Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Ajali mbaya kuliko zote duniani Kiroho

Hizi ndio ajali mbaya kuliko zote hapa Duniani, japo wengi huziona za kawaida tu, omba usikutane nazo kabisa!.. soma zaidi

a.gif Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;.. soma zaidi

a.gif Misa Takatifu hutolewa kwa ajili ya nani?

Misa Takatifu hutolewa kwa ajili ya kanisa nzima yaani kwa ajili ya watu wote wazima na wafu. (Ebr 9:14. Rum 1:9).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 19, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 19, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA MAPENDO

[Wimbo Mzuri PA.gif] Bwana Nakushukuru Asante

[Tafakari ya Sasa] 👉Jambo la muhimu zaidi Duniani

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

KADI-MSAMAHA-MZAZI.JPG

a.gif Sakramenti ya Mpako Wa Wagonjwa inamanufaa gani rohoni mwa mtu?

Manufaa ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni.. soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu… soma zaidi

a.gif Mafundisho kuhusu Karama

Mambo ya muhimu kujua kuhusu Karama;.. soma zaidi

a.gif Kuzaliwa kwa Isaka

1 Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema… soma zaidi

a.gif Amri ya saba ya Mungu inakataza nini?

Inakataza haya;.. soma zaidi

a.gif Watawa wanashika mashauri gani ya Kiinjili?

Watawa wanashika hasa mashauri ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu ambayo msingi wake ni maisha na mafundisho ya Yesu kadiri ya Injili… soma zaidi

a.gif Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.. soma zaidi

a.gif Mungu ni nani? Sifa za Mungu

Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote, katika mbingu na nchi, Mkubwa wa Ulimwengu mwenye kuwtunza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya. (Mt: 6:8-9, Yoh 20: 17).. soma zaidi

a.gif Picha ya Huruma ya Mungu

Bwana Yesu alianza kumtokea Sista Faustina mfululizo tangu mwaka 1930 hadi 1938. Alimtokea ili kumwandaa kwa ujumbe mkubwa wa maisha wa kuitgazia dunia nzima ibada ya Huruma ya Mungu, ambayo ilikuwa na madhumuni yafuatayo;

  • Kuandaa ujio wa Pili wa Bwana wetu Yesu Kristo aliye Mfalme wa Huruma.
  • Kuokoa roho zilizoko Toharani.
  • Kuwaongoa wakosefu ambao wameshapoteza neema ya kujiombea.
  • Kuitangaza Huruma ya Mungu… soma zaidi

a.gif Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?

Ndiyo, “ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” (Zab 116:15)… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.