MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 12, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

Somo la Kwanza

Mwa 46 :1-7, 28-30

Israeli alisafiri pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha lena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao, na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua. Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye. Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri. Yakobo akampeleka Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni. Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake, kitambo kizima. Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.

Wimbo wa katikati

Zab 37 :3-4, 18-19, 27-28, 39-40

Umtumaini Bwana ukatende mema,
ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
Nawe utajifurahisha kwa Bwana,
naye atakupa haja za moyo wako.
(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana.

Bwana anazijua siku za wakamilifu,
na urithi wao utakuwa wa milele.
Hawataaibika wakati wa ubaya,
na siku za njaa watashiba.
(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana.

Jiepue na uovu, utende mema,
na kukaa hata milele.
Kwa kuwa Bwana hupenda haki,
wala hawaachi watauwa wake.
(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana.

Na wokovu wenye haki una Bwana,
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
Naye Bwana huwasaidia na kuwaopoa,
huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa,
kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana.

Shangilio

Yak 1:21

Aleluya, aleluya,
Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.

Somo la Injili

Mt 10:16-23

Yesu aliwaambia mitume wake: Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua. Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa. Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema. Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu. Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.


a.gif Majuto kamili ni nini?

Majuto kamili ni kujuta kwa sababu tumemchukiza Mungu mwenyewe aliye mwema na mpendelevu kabisa.. soma zaidi

a.gif Siku Sita za Mungu kuumba Dunia

1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi… soma zaidi

a.gif Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?

Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 12, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 12, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala ya Malaika w Bwana

[Tafakari ya Sasa] 👉Uwe na subira Baada ya kuomba

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Maria Goretti

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

KADI-MZAZI-ASUBUHI.JPG

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ni fadhila gani inayoondoa majivuno?

Fadhila inayoondoa majivuno ni fadhila ya Unyenyekevu.. soma zaidi

a.gif Nani aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi?

Musa ndiye aliwatoa Waisraeli MIsri na Kuwaongoza Katika nchi ya Ahadi.. soma zaidi

a.gif Ushauri wangu kwa leo, ni Heri kuchagua kunyamaza

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi

a.gif Tunawaheshimu Watakatifu namna gani?

Tunawaheshimu kwa kuadhimisha sikukuu zao, kwa kuomba maombezi yao, kufuata mifano yao na kuheshimu masalia na sanamu zao, kwa kuinama kichwa kidogo tunapopita mbele yake.. soma zaidi

a.gif Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu… soma zaidi

a.gif Kwa nini tujute dhambi zetu?

Tunajuta dhambi zetu kwa sababu tumeukosea Utatu Mtakatifu na tunastahili adhabu yake, na pia bila majuto hatuwezi kupata maondoleo ya dhambi… soma zaidi

a.gif Je, Maria ni mama yetu pia?

Ndiyo, Maria ni mama yetu pia: kwa kushiriki kazi yote ya Mwanae, Adamu mpya, amekuwa Eva mpya, mama wa wale wote aliowakomboa msalabani… soma zaidi

a.gif Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?

Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu… soma zaidi

a.gif Mambo ya Msingi Unayopaswa kufahamu kuhusu Ekaristi Takatifu: Mwili na Damu Ya Bwana Wetu Yesu Kristu

Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, katika
maumbo ya mkate na divai. Sakramenti hii
iliwekwa na Yesu Mwenyewe kwenye karamu ya mwisho, siku ya Alhamisi jioni kabla ya mateso
yake. (Yoh 6:1-71; Mt 26:26-28)... soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.