MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JUNI 27, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Kanisa Katoliki ni nini?

Somo la Kwanza

Mwa 16:1-12, 15-16

1Basi, Sarai, mkewe Abramu, alikuwa bado hajamzalia mumewe mtoto. Lakini alikuwa na mjakazi aliyeitwa Hagari, kutoka Misri. 2Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.

3Kisha, Sarai akampa Abramu Hagari, mjakazi wake ambaye alikuwa Mmisri, awe mke wake. Haya yalitokea baada ya Abramu kukaa katika nchi ya Kanaani kwa muda wa miaka kumi. 4Abramu akamchukua Hagari, naye Hagari akapata mimba. Lakini mara tu alipoona amepata mimba, Hagari akaanza kumdharau bimkubwa wake.

5Sarai akamwambia Abramu, “Wewe utawajibika kwa ubaya ninaotendewa. Mimi nilikupa mjakazi wangu, lakini alipopata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake! Mwenyezi-Mungu na ahukumu kati yako na mimi!” 6Lakini Abramu akamwambia Sarai, “Mjakazi wako yuko chini ya mamlaka yako; mfanyie upendavyo.” Basi, Sarai akamtesa Hagari mpaka akatoroka.

7Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamkuta Hagari penye chemchemi ya maji jangwani, chemchemi iliyoko njiani kuelekea Shuri. 8Malaika akamwuliza, “Hagari, mjakazi wa Sarai! Unatoka wapi na unakwenda wapi?” Hagari akamjibu, “Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.” 9Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Rudi kwa bimkubwa wako Sarai na umtii.” 10Zaidi ya hayo, malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Hagari, “Nitawazidisha wazawa wako hata wasiweze kuhesabika kwa wingi wao.” 11Kisha huyo malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Wewe ni mjamzito na utajifungua mtoto wa kiume; utamwita Ishmaeli, maana Mwenyezi-Mungu amesikia mateso yako.

12Ishmaeli ataishi kama pundamwitu; atakuwa adui wa kila mtu na kila mtu atakuwa adui yake. Ataishi akiwa adui wa jamaa yake.”

15Hagari akamzalia Abramu mtoto wa kiume. Abramu akamwita mtoto huyo Ishmaeli. 16Abramu alikuwa na umri wa miaka 86 wakati Hagari alipomzaa Ishmaeli.

Wimbo wa katikati

Zab 105:1-5

1Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake;
yajulisheni mataifa mambo aliyotenda!
2Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa;
simulieni matendo yake ya ajabu!
3Jisifieni jina lake takatifu;
wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi.
4Tafuteni msaada kwa Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu;
mwendeeni Mwenyezi-Mungu daima.
5Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda,
miujiza yake na hukumu alizotoa,

Somo la Injili

Mt 7:21-29

21“Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni. 22Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. 23 Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’

24“Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. 25Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.
26“Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. 27Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena anguko hilo lilikuwa kubwa.”

28Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake. 29Hakuwa kama waalimu wao wa sheria, bali alifundisha kwa mamlaka.


a.gif Kuna majuto ya namna ngapi?

una majuto ya namna mbili,
1. Majuto kamili/Majuto ya mapendo
2. Majuto yasiyokamili/majuto pungufu/majuto ya hofu.. soma zaidi

a.gif Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?

Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo… soma zaidi

a.gif Sikukuu Kubwa Kupita zote Katika Kanisa ni ipi?

Sikukuu Kubwa Kupita zote Katika Kanisa ni PASAKA.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JUNI 27, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JUNI 27, 2019: JUMA LA 12 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu anajibu sala kutokana na nia

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Jorome

msaada.gif

a.gif Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?

Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo.. soma zaidi

a.gif Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu gani?

Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika utamaduni wake na katika Agano la Kale… soma zaidi

a.gif Mtume aliyechaguliwa na Mitume badala ya Yuda iskarioti

Alikua ni Mtume Mathia.. soma zaidi

a.gif Zingatia hili kuokoa nafsi yako

Kundi la watu lilikwenda mahali wakakuta mawe yamezagaa. Ghafla wakasikia sauti ikisema: "Atakaeokota atajuta na asiyeokota atajuta,".. soma zaidi

a.gif Watawa wanashika mashauri gani ya Kiinjili?

Watawa wanashika hasa mashauri ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu ambayo msingi wake ni maisha na mafundisho ya Yesu kadiri ya Injili… soma zaidi

a.gif Chini ya Uongozi wa Kanisa Katekista anafanya Kazi gani?

1. Yeye ni Kiungo cha Mapadre na waamini wa eneo lake
2. Kufikisha mafundisho ya Injili na kuhusika kwenye kazi za Ibada za kiliturujia na kazi za Huruma
3. Kuhubiri na kuwafundisha wakatekumeni
4. Kuelimisha vijana na watu wazima kkatika maswala ya Imani.. soma zaidi

a.gif Ndoa ya utofauti wa Imani maana yake ni nini?

Ndoa ya utofauti wa Imani ni ndoa kati ya Mkristo Mkatoliki na mtu ambaye hajabatizwa kwa mfano Mpagani, Mwislamu, Yehova, Mlokole tangu kuzaliwa n.k.. soma zaidi

a.gif Sala zipo za namna ngapi?

Sala zipo za namna tatu,.. soma zaidi

a.gif Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima.. soma zaidi

a.gif Maana ya baraka ni ipi?

Maana ya baraka ni kumsifu Mungu kwa yale aliyokwishatujalia na kumuomba azidi kutujalia kadiri ya mahitaji ya wahusika. Mara nyingi inatolewa na mtu mwenye daraja au mamlaka fulani… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.