MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 4, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 4, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

SOMO 1

Mwa 22:1-19

Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali. Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na Kuwarudia tena.

Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja, Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babaangu! Naye akasema, Mimi hapa mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo,lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi waka endelea wote wawili pamoja.

Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinge mwanawe.

Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana; mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana; sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee. Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pemba zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa Bwana itapatikana.

Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu pili kutoka mbinguni, akasema, Nimeapa kwa nafasi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda nenno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kumilikizidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umeti sauti yangu. Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 116 :1-6, 8-9 (K) 9

(K) Nitaenenda mbele za Bwana katika nchi za walio hai

Aleluya.
Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza
Sauti yangu na dua zangu
Kwa maana amenitegea sikio lake,
Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. (K)

Kamba za mauti zilinizunguka,
Shida za kuzimu zilinipata.
Naliona taabu na huzuni;
N’ikaliitia jina la Bwana.
Ee Bwana, nakuomba sana,
Uniokoe nafsi yangu. (K)

Bwana huwalinda wasio na hila;
Naliadhilika, akaniokoa.
Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako,
Kwa kuwa Bwana amekutenda ukarimu. (K)

Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,
Macho yangu na machozi,
Na miguu yangu na kuanguka.
Nitaenenda mbele za Bwana
Katika nchi za walio hai. (K)

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Mbegu ni neno la Mungu,
anayepanda ni Kristo.
atakayemkuta, ataishi milele.
Aleluya.

INJILI

Mt. 9:1-8

Yesu alipanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao. Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu; umesamehewa dhambi zako. Na tazama. Baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. Naye Yesu hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu? Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii.

Injili ya Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Maisha ya Mtoto Yesu huko Nazareth yanatufundisha nini?

Yanatufundisha kuishi kwa uaminifu, kufuata malezi bora, kuwatii wazazi, walezi na wakubwa zetu. (Lk 2:51, Rum 13:1).. soma zaidi

a.gif Novena ya Huruma ya Mungu

Utangulizi.. soma zaidi

a.gif Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 4, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 4, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa Malaika Mlinzi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kando ya mito ya babeli

[Tafakari ya Sasa] 👉Njia ya Kumrudia Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Teresa (Teresia) wa Yesu (Avila)

UJUMBE-HONGERA-NDUGUU.JPG

a.gif Kwa nini ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo?

Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila tunapofanya ukumbusho wa sadaka hiyo pekee tunazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu “ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yoh 13:1)... soma zaidi

a.gif Ni fadhila gani inayoondoa majivuno?

Fadhila inayoondoa majivuno ni fadhila ya Unyenyekevu.. soma zaidi

a.gif Je, ni muhimu tujiandae kufa?

Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Eb 9:27)… soma zaidi

a.gif Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kufanya nini?

Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila ya mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua… soma zaidi

a.gif Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;.. soma zaidi

a.gif Tumuadhimishe nani?

Tumuadhimishe Mungu pekee siku zote za maisha yetu kwa tumaini la kumuadhimisha milele… soma zaidi

a.gif Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Uaminifu

Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu… soma zaidi

a.gif Malaika wema kazi yao ni nini?

Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika wetu Walinzi. (Ebr 13:2).. soma zaidi

a.gif Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.