MASOMO YA MISA, ALHAMISI,, JULAI 25, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Kanisa linahusika vipi na imani?

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, ALHAMISI,, JULAI 25, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

SIKUKUU YA MT. YAKOBO, MTUME

SOMO 1

2 Kor. 4 : 7-15

Tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi; siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. Kwa maana sisi tulio hai, sikuzote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti. Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu.

Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa, Naliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini, na kwa sababu hiyo twanena; tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi. Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe.

Neno la Mungu…Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 126 (K) 5

(K) Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.

Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni,
Tulikuwa kama waotao ndoto.
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,
Na ulimi wetu kelele za furaha. (K)

Ndipo waliposema katika mataifa,
Bwana amewatendea mambo makuu.
Bwana alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa tukifurahi. (K)

Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa,
Kama vijito vya Kusini.
Wapandao kwa machozi
Watavuna kwa kelele za furaha. (K)

Ingawa mtu anakwenda zake akilia,
Azichukuapo mbegu za kupanda.
Hakika atarudi kwa kelele za furaha,
Aichukuapo miganda yake. (K)

SHANGILIO

Yn. 15: 16

Aleluya, aleluya, Ni mimi niliyewachagua ninyi nikawaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kukaa, asema Bwana. Aleluya.

INJILI

Mt. 20 :20-28

Mama yao wana wa Zebedayo alimwendea Yesu pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno. Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekwa tayari na Baba yangu.

Na wale kumi waliposikia, waliwakasirikia wale ndugu wawili. Lakini Yesu akawaita, akasema Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Maswali na majibu kuhusu Watakatifu ndani ya Kanisa Katoliki

Soma haya kuhusu watakatifu;.. soma zaidi

a.gif Ni ishara gani zinazoshuhudia ufufuko wa Yesu?

Ni ishara zifuatazo;.. soma zaidi

a.gif Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;

  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu.. soma zaidi


Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, ALHAMISI,, JULAI 25, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, ALHAMISI,, JULAI 25, 2019: JUMA LA 16 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE 1

[Tafakari ya Sasa] 👉Mkono wa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Klara wa Asizi

KWA-NINI-BIKIRA-MARIA-ANAPEWA-HESHIMA.JPG

a.gif Vitabu vya manabii katika Biblia ni vipi?

Vitabu vya Manabii ni
1. Isaya
2. Yeremia
3. Maombolezo
4. Baruku
5. Eekieli
6. Danieli.. soma zaidi

a.gif Neema ya Msaada ni nini?

Neema ya Msaada ni msaada tupatao kwa Roho Mtakatifu kutuongezea nguvu Rohoni tutende mambo mema na tuepuke Mabaya.. soma zaidi

a.gif Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22)… soma zaidi

a.gif Dhana ya kusema ukweli Daima katika Maisha ya kila siku ya Mkristo

🔧KUKAZIA MAARIFA🔩
đź“ŤKatika tafakari ya juzi, tuligusia wajibu wetu-kimaadili wa kusema ukweli na ukweli mtupu kwa sababu neno la Mungu linasema "usiseme uwongo na tena …uvueni uongo mkaseme kweli…". Hivyo NI LAZIMA KUSEMA UKWELI KWA MOYO… soma zaidi

a.gif Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;.. soma zaidi

a.gif Je, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu. Yesu aliyesema, “Sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17), alifuata kalenda ya dini ya Kiyahudi, halafu kwa kufa na kufufuka amekuwa kiini cha ibada zetu zote. Hivyo Mitume waliadhimisha siku aliyofufuka kama “siku ya Bwana” (Ufu 1:10) ambapo wakutane “ili kumega mkate” (Mdo 20:7) wa ekaristi… soma zaidi

a.gif Wakati sahihi wa kumuomba Mungu akupe Mume/Mke

👉NI WAKATI GANI SAHIHI KUOMBA MUNGU ANIPE MKE /MUME?
JIBU…. soma zaidi

a.gif Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu? Na kwa nini aheshimiwe?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu kwa sababu amemzaa Yesu na Yesu ni Mungusoma zaidi

a.gif Siku za kufunga ni zipi? Na siku gani tumekatazwa kula nyama?

Siku za kufunga ni Jumatano ya majivu, siku za Kwaresima isipokuwa Dominika zake, na siku iliyokatazwa kula nyama ni siku ya Ijumaa kuu… soma zaidi

a.gif Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.