MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 18, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Kut. 3:13-20

Musa alimwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza. Jina lake n’nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, Mimi niko ambaye niko; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; Mimi niko amenituma kwenu.
Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.

Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri; Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misrei na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali. Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, Bwana, Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo wa siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu Bwana, Mungu wetu. Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu. Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 105:1, 5, 8-9, 24-27 (K) 8

(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Aleluya.
Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake. (K)

Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilolifanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka. (K)

Akawajalia watu wake wazae sana,
Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.
Akawageuza moyo wawachukie watu wake,
Wakawatendea hila watumishi wake. (K)

SHANGILIO

Zab. 19:8

Aleluya, aleluya,
Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.

INJILI

Mt. 11:28 – 30

Yesu aliwaambia makutano: Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, name nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Je, vitabu vya Biblia vinatofautiana?

Ndiyo, vitabu vya Biblia vinatofautiana kwa kuwa Mungu alijifunua hatua kwa hatua; hivyo vitabu 46 vilivyoandikwa kabla ya Yesu vinaitwa Agano la Kale na 27 vilivyomfuata vinaitwa Agano Jipya… soma zaidi

a.gif Maana kamili ya Kwaresma

Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40). Mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu… soma zaidi

a.gif Kwa nini Wakatoliki wanaungama dhambi kwa Padri?

KWANINI NYIE WAKATOLIKI MNAUNGAMA DHAMBI KWA PADRE AMBAYE NI MWANADAMU NA MDHAMBI BADALA YA KUUNGAMA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU?.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 18, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 18, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Majitoleo ya Asubuhi

[Tafakari ya Sasa] 👉Furaha ya Binadamu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Malaika wakuu wako watatu ambao ni?

Malaika wakuu wako watatu: Mikaeli, Raphaeli na Gabrieli (Dn 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26).. soma zaidi

a.gif Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu.. soma zaidi

a.gif Tupendane

Wapenzi tupendane,.. soma zaidi

a.gif Maana ya jina Bikira Maria

Jina asili kwa Kiaramu ni מרים, Maryām lenye maana ya "Bibi"; watafsiri wa kwanza wa Biblia ya Kiebrania wanaojulikana kama Septuaginta (LXX) waliliacha kama lilivyo wakiandika kwa Kigiriki Μαρίαμ, Mariam, au walilifupisha wakiandika Μαρία, Maria… soma zaidi

a.gif Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?

Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15).. soma zaidi

a.gif Je, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu?

Ndiyo, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu na kulenga hasa kuandaa watu wampokee, wamfuate na kumshuhudia katika umoja wa kundi lake, Kanisa… soma zaidi

a.gif Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?

Msimamizi wa ubatizo ana wajibu hizi;.. soma zaidi

a.gif Katika Amri ya Sita na Tisa Mungu ametuamuru nini?

Mungu ametuamuru kutunza usafi wa moyo na kuwa waaminifu katika ndoa… soma zaidi

a.gif Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake… soma zaidi

a.gif Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.