MASOMO YA MISA, AGOSTI 3, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 17 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?


MASOMO YA MISA, AGOSTI 3, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 17 LA MWAKA

SOMO 1

Wal. 25:1,8-17

Bwana alinena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia: Utajihesabia sabato za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote waiketio; itakuwa ni yubile kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabihu za mizabibu isiyopelewa. Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.
Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. Tena kama ukimwuzia jirani yako chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 67:1-2, 4- 6-7 (K) 3

(K) Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru.

Mungu na atufadhili na kutubariki,
Na kutuangazia uso wake.
Njia yake ijulikane duniani,
Wokovu wake katikati ya mataifa yote. (K)

Mataifa na washangilie,
Naam, waimbe kwa furaha,
Maana kwa haki utawahukumu watu,
Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. (K)

Nchi imetoa mazao yake;
Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
Mungu atatubariki sisi;
Miisho yote ya dunia itamcha Yeye. (K)

SHANGILIO

Zab. 25:4,5

Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.

INJILI

Mt. 14:1 – 12

Mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake, Huyo ndiye Yohane Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake.
Maana Herode alikuwa amemkamata Yohane, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye. Kwa sababu Yohane alimwambia, Si halali kwako kuwa naye. Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohane kuwa nabii. Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Heorode. Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lolote atakaloliomba. Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohane Mbatizaji.
Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; akatuma mtu akamkata kichwa Yohane mle gerezani. Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye. Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Kati ya sanaa kwenye ibada/kumuadhimisha Mungu, muhimu zaidi ni ipi?

Kati ya sanaa, muhimu zaidi ni uimbaji, kwa kuwa unahusiana zaidi na Neno la Mungu, ukilitia maanani kwa uzuri wa muziki. Katika Agano la Kale, kitabu cha Zaburi ni nyimbo tupu za kutumia katika ibada… soma zaidi

a.gif Mafundisho kuhusu Karama

Mambo ya muhimu kujua kuhusu Karama;.. soma zaidi

a.gif Mungu anakupenda

Nani kama Mungu?.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, AGOSTI 3, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 17 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, AGOSTI 3, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 17 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwenye Huruma

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

a.gif Ni fadhila gani inayoondoa ubahili?

Fadhila inayoondoa ubahili ni ukarimu.. soma zaidi

a.gif Utafuteje dhambi wakati wa kujiandaa kuungama?

Tafuta dhambi kwa njia hizi.. soma zaidi

a.gif Rehema kamili ni nini?

Rehema kamili ni msamaha wa kufutiwa adhabu zote za muda za dhambi.. soma zaidi

a.gif Tabernakulo ni nini?

Tabernakulo ni mahali Patakatifu anapokaa Yesu wa Ekaristi siku zote.. soma zaidi

a.gif Je, divai (pombe) ni halali?

Ndiyo, divai ni halali, mradi itumike kwa kiasi isije ikaleta madhara… soma zaidi

a.gif Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna “ubatizo mmoja” (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya “kwa maji na kwa Roho” (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa… soma zaidi

a.gif Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu… soma zaidi

a.gif Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu ngapi?

Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu tatu.. soma zaidi

a.gif Akili ni nini?

Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu.. soma zaidi

a.gif Motoni ni nini?

Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.