A MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 1, 2019: DOMINIKA YA 22 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

YbS 3:17 – 20, 28 -29

Mwanangu, wakati wa kufanikiwa uendelee katika unyenyekevu; hivyo utapendwa kuliko mwenye ukarimu. Kadiri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha, nawe utapata kibali machoni pa Bwana; kwa maana rehema zake Bwana zi kuu, na siri yake ni kwa wanyenyekevu.

Msiba wa mwenye kiburi hauleti kupona, Mche wa uovu umepandika ndani yake. Moyo wa busara utatambua mithali, Na sikio sikivu ni tamaa ya mtaalamu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 68:3 – 6, 9 – 10 (K) 10

(K) Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa.

Wenye haki watafurahi,
Na kushangilia uso wa Mungu;
Naam, watapiga kelele kwa furaha.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake.
Furahini katika Bwana, shangilieni mbele zake. (K)

Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu katika kao lake takatifu.
Mungu huwakalisha wapweke nyumbani,
Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa. (K)

Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema,
Urithi, urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
Kabila lako lilifanya kao lake huko,
Ee Mungu,
Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa. (K)

SOMO 2

Ebr. 12:18 – 19, 22 – 24

Hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliwaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lolote linguine. Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Mt. 11:25

Aleluya, aleluya,
Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi,
kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, Ukawafunuliwa watoto wachanga.
Aleluya.

INJILI

Lk. 14:1, 7 – 14

Yesu alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe nay eye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele Zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo


a.gif Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo… soma zaidi

a.gif Anayeharibu mali ya mwingine lazima afanye nini?

Anayeharibu mali ya mwingine lazima alipe hasara aliyosababisha. (Lk 19:8).. soma zaidi

a.gif Kanisa linamuadhimishaje Mungu tena?

Kanisa linamuadhimisha Mungu tena kwa visakramenti ambavyo kwa mamlaka ya Kristo linawatia watu neema zake katika nafasi yoyote ya maisha. Kati yake muhimu zaidi ni baraka na mazinguo, ambavyo vipo tangu zamani, hata nje ya taifa la Israeli… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya A MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 1, 2019: DOMINIKA YA 22 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; A MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 1, 2019: DOMINIKA YA 22 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Zaeni matunda mema

[Tafakari ya Sasa] 👉Kutubu na Kusamehewa dhambi

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Fransisko wa Sales

[Jarida La Bure] 👉NOVENA YA ROHO MTAKATIFU

misaadas.gif

a.gif Katika Amri ya nne ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tuwaheshimu wazazi wetu na wakubwa wetu wote, tuwapende, tuwatii na tuwaombee. (Kut 20:12, Kol 3:20).. soma zaidi

a.gif Ni vitu gani vya msingi na vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu?

Vitu vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu ni.. soma zaidi

a.gif Watu wa jinsia moja waweza kuoana?

Hapana, watu wa Jinsia moja hawawezi kuoana na wakifanya hinyo wanatenda dhambi kubwa inayomlilia Mungu. (Wal 18:22).. soma zaidi

a.gif Mashahidi na Wafiadini wa Uganda

Nchi ya Uganda iliwahi kupatwa na dhuluma  dhidi ya  dini, hasa  Ukristo, hususan  madhehebu  ya  Anglikana  na Kanisa Katoliki. Waliouawa katika mazingira ya namna hiyo, wanaitwa wafiadini/mashahidi… soma zaidi

a.gif Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane… soma zaidi

a.gif Yuda Iskarioti

Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), Myahudi wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16)… soma zaidi

a.gif Watoto wawili wa Adamu na Eva walkikuwa wepi?

Walikuwa ni Kaini na Abeli.. soma zaidi

a.gif Mafundisho kuhusu Vilema, Vichwa vya dhambi au mizizi ya dhambi

Kuhusu vilema au vichwa vya dhambi soma haya;.. soma zaidi

a.gif Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha

Yesu ni Mwanga na Uovu ni giza.. soma zaidi

a.gif Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.