Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume

Vifaa vya kieletroniki

Vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Usiweke simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia.

Vile vile usitumie masaa mengi kwenye kompyuta.

Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya

Mfano wireless internet au Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation).

Uvutaji wa Sigara

Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume.

Viuavijasumu, Viuatilifu na homoni katika vyakula

– Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Aina ya chakula

Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku. Hasa vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

Kujichua (punyeto)

Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Vyakula vyenye soya

Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume.

Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.

Unywaji pombe

Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

Joto kupita kiasi (Hyperthermia)

Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya.

Joto kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

Mfadhaiko (Stress)

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Vitu vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume;

a.gif Mambo ya kuzingatia kujikinga na chunusi | Jinsi ya kuzuia

1. Fanya mazoezi ya viungo kwa saa moja kila siku
2. Kunywa maji mengi kila siku
3. Ondoa mfadhaiko (stress)
4. Weka homoni sawa kama hazipo sawa
5. Kuwa msafi wa mwili wote kila mara
6. Usiziguse chunusi au kuzitoboa na mikono yako au na chochote kuepuka makovu yasiyo ya lazima
7. Epuka vyakula vifuatavyo kama unasumbuliwa na chunusi kila mara, navyo ni pamoja na:.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Mtindi na asali

Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi… endelea kusoma

a.gif Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Juisi Ya Mabungo

Mahitaji.. endelea kusoma

[Picha Nzuri] 👉Huyu kawezwa, Ringa tena

[Msemo wa Leo] 👉Mke Na Mme Kusaidiana

[Jarida la Bure] 👉Picha Kali Za Kuchekesha

[SMS kwa Umpendaye] 👉Ujumbe mzuri wa salamu kwa mpenzi wako

a.gif Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)

Mboga za majani makavu ¼ kg
Mafuta vijiko vikubwa 3-4
Karanga zilizosagwa kikombe ½
Maziwa au tui la nazi kikombe 1
Kitunguu 1
Nyanya 2
Chumvi (kama kuna ulazima)
Maji baridi.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga Mchanganyiko

Mchele - 2 Mugs.. endelea kusoma

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png
SALAMU-ASUBUHI-987HGZ.JPG
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.