Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ kwa punguzo kutoka Tsh 6500/= hadi Tsh 2500/= kwa leo tuu!.
👉<<Bofya hapa Kuoda>> Kizuri

.

👉 Virutubishi, kazi zake katika mwili na vyanzo vyake

Virutubishi

ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishi vya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.

Aina za virutubishi vinavyohitajika mwilini

  1. Kabohaidreti / vyakula vya wanga
  2. Mafuta ya Wanyama na Mimea
  3. Protini
  4. Vitamini na Madini
  5. Maji

Kabohaidreti / vyakula vya wanga

Kabohaidreti / vyakula vya wanga huvipa mwili nguvu inayoihitajika kujiendesha. Vyakula
hivi vyaweza kuwa sahili au changamani. Hii inahusu jinsi ambavyo chakula chaweza
kubadilisha sukari katika mwili. Vyakula vya wanga na sukari huvipa mwili nguvu
inayohitajika kuufanya upumue na kuendelea kuishi, kuwa na mwendo na utoaji joto, na kwa
ukuaji na utengenezaji wa mkusanyiko wa seli (tishu). Baadhi ya wanga na sukari
hubadilishwa kuwa mafuta mwilini.
Ufumwele utokanao na kabohaidreti hufanya kinyesi kiwe laini na kingi na huondoa kemikali
za sumu, na hivyo hufanya matumbo yawe na afya njema. Hupunguza uyeyushaji na
ufyonzaji wa virutubishi katika vyakula, na husaidia kupunguza unene.

Vyanzo vya kabohaidreti

Vyanzo vikuu vya kabohaidreti ni:

• Nafaka

- Mahindi/ugali
- Serena
- Mtama
- Mchele
- Unga wa ngano

• Mizizi ya vyakula vya wanga

- Viazi vitamu
- jimbi
- Viazi mviringo
- Muhogo mbichi
- Unga wa muhogo
- Ndizi

Mahitaji ya kabohaidreti mwilini

- Mahitaji hutofautiana kutegemea na umri, jinsi, jinsia, shughuli, hali ya kiafya
- Kula mara tatu au zaidi kwa siku.

Mafuta ya Wanyama na Mimea

Mafuta ya wanyama na mimea kwenye chakula na tishu ya shahamu kwenye miili yetu huwa
na shughuli nyingi

Kazi za mafuta ya wanyama kwenye mwili

Virutubishi: mafuta ya wanyama hutoa tindikali za mafuta muhimu, ambazo
huhitajika katika ukuaji wa kawaida kwa watoto wachanga na watoto wengine na
kwa uzalishaj wa michanganyiko ya aina ya kihomoni inayorekebisha upeo mpana
wa shughuli za kimwili na kukufanya uwe mwenye afya njema.
Usafirishaji: mafuta ya wanyama hubeba mafuta ya miyeyusho ya vitamini (A, D,
E, na K) na kurahisisha ufyonzaji wake.
Ufahamu: mafuta ya wanyama huchangia kwenye harufu nzuri na ladha ya
chakula.
Umbile la asili: mafuta ya wanyama hufanya chakula (hususan nyama na vyakula
vya kukaushwa) kuwa nyororo.
Ukinaishaji: mafuta ya wanyama hukipa chakula ukinaishaji, hivyo hujikuta
umeshiba na kutosheka kwa muda mrefu baada ya chakula.
Mafuta ya wanyama ni chanzo cha utoaji wa mkusanyiko wa kalori. Hili ni jambo
jema unapokuwa kwenye safari ndefu, itumiayo nguvu nyingi, ukiwa umebeba
chakula chako.

Mafuta ya wanyama mwilini hufanya yafuatayo:

• Mafuta ni muundo mkuu wa mwili wa kuhifadhi nishati (ambazo ni muhimu wakati wa
ugonjwa au kupungua kwa ulaji chakula)
• Mafuta hutoa sehemu kubwa ya nishati inayotumika kwenye kufanyiza kazi misuli.
• Mafuta hukinga viungo vya ndani na kuhami miili yetu dhidi ya hali za joto
zinazopitiliza mipaka.
• Mafuta huunda malighafi kuu ya utando wa seli (hususan seli za ubongo na za
mishipa ya fahamu)
• Mafuta hugeuzwa kuwa aina nyingi za homoni (ikiwemo homoni za mambo yahusuyo
mapenzi)
Mafuta ki kitu kizuri! Isipokuwa tu pale uzuri unapozidi kiwango ndipo kunapokua na tatizo.

Aina za mafuta:

mafuta yaliyokolea dhidi ya yale yasiyokolea
Kama ambavyo kuna aina kuu mbili za kabohaidreti, kuna aina kuu mbili za mafuta
kutegemea na mfumo wake wa kikemia; mafuta yaliyokolea na yale ambayo hayajakolea.
Aina hizi za mafuta zina athali tofauti kabisa kwa afya yako.

1. Mafuta yaliyokolea

• Huwa na kawaida ya kuongeza lehemu “mbaya” kwenye damu na kuongeza
uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo.
• Mafuta yaliyokolea huwa na kawaida ya kuganda kwenye hali ya joto la kawaida.
• Hupatikana kwa wingi kutokana na vyanzo vya mafuta ya wanyama.
Vyanzo vya mafuta yaliyokolea
• Siagi, malai, mafuta ya nyama ya ngómbe, ngozi ya kuku, mafuta ya maziwa yenye
malai, jibini, aisikirimu, siagi, samli, mafuta ya nguruwe/ya kupikia, mafuta
yatokanayo na nyama, mawese mekundu, na nazi.
• Yaliyopo nje ya utaratibu: mafuta ya nchi za joto (ikiwemo ya nazi na mawese) yana
kiwango kikubwa cha mafuta yaliyokolea.

2. Mafuta yasiyokolea

• Mafuta yasiyokolea ni aina ya mafuta ambayo kwa ujumla yanahusishwa na afya bora.
• Yana kwaida ya kushusha viwango vya lehemu na kupunguza hatari za magojwa ya
moyo.
• Mafuta yasiyokolea huwa na kawaida ya kuwa ya mmiminiko katika joto la kawaida.
• Hupatikana kwa wingi kutokana na mimea.
Vyanzo vya mafuta yasiyokolea
• Mafuta yatokanayo na mboga za majani, mizeituni, miparachichi, njugu, mafuta ya
karanga, maharagwe meupe, mbegu za alizeti, mbegu za ufuta na aina nyingine za
mbegu, mafuta ya samaki na soya.
• siagi, samli, mafuta ya nguruwe/ya kupikia, maziwa yenye malai, jibini, mafuta
yatokanayo na nyama, mawese mekundu, na nazi.

Kuna mafuta yatokanayo na kuchujwa kwa mafuta ya mbogamboga na kugandishwa. Mafuta
haya huishia kuwa na tabia za mafuta yaliyokolea. Mafuta haya pia hayapashwi kutumiwa
kwa wingi.

Vyanzo ni:

• majarini, mafuta ya nguruwe, vyakula vya kukaangwa, donati, keki, biskuti, aiskrimu.

Mahitaji ya mafuta mwilini

Mahitaji ya mafuta huelezewa kama ‘ni asilimia ya mahitaji yote ya nishati’. Kiwango chote
cha asilimia ya nishati kinachopashwa kitokane na mafuta katika mlo bora uliokamilika ni
kama ifuatvyo:
• Asilimia 30-40 kwa watoto hadi kufikia miaka miwili kwenye milo ya nyongeza
• Asilimia 15-30 kwa watoto wakubwa na wengi wa watu wazima; kwa watu wazimu
wenye afya - hadi asilimia 35 inakubalika.
• Angalau asilimia 20 hadi 30 kwa akina mama wenye umri wa kuweza kuzaa (15-45).

Protini

Protini ni zana za ujenzi wa misuli yetu, viungo na baadhi ya vitu vingi vinavyotengeneza
miili yetu. Hutoa tindikali muhimu za amino zitumiwazo na mwili kutengeneza misuli ya tishu.
Mwili unahitaji protini na kalori kila siku.
Unapokosa kupata kalori na protini za kutosha kila siku, mwili wako hutumia akiba yake
kufidia pengo la ukosefu wa nishati. Hali hii huinyima mwili wako kalori unazohitaji kuufanya
uwe na afya bora na hivyo kusababisha kupungua kwa uzito.

Vyanzo vya protini

Protini yaweza kupatikana kwenye vyakula vya wanyama na mimea.

1. Vyanzo vitokanavyo na wanyama

• Nyama, kuku/mabata n.k., samaki, mayai, jibini, maziwa na mtindi.
• Vyakula hivi vinachukuliwa kuwa kama ‘kamili’ au ‘vyenye kiwango cha juu’cha
protini kwa kuwa vina aina zote za ‘tindikali muhimu za amino’. ‘Muhimu”inamaanisha
lazima vitumiwe kwenye milo yetu; miili yetu haiwezi kuzitengeneza.

2. Vanyzo vitokanavyo na mimea

• Bidhaa zitokanazo na soya, (tofu, tempeh), maziwa ya soya na mazao mengine
yatengenezwayo na soya), maharagwe, mbegu na njugu.
• Viwango vidogo vya protini vinapatikana vilevile kwenye mikate, mahindi /ngano, na
aina nyinge ya nafaka, na mbogamboga pia.
• Vyanzo hivi vya protini vinachukuliwa kama ‘si kamili’kwa kuwa vinakosa moja au
zaidi ya tindikali muhimu za amino.
• Protini ya maharagwe meupe ndiyo ya kipekee. Haya yanachukuliwa kuwa ni kamili.

Mahitaji ya protini mwilini

Mahitaji hutofautiana kulingana na umri, jinsi, jinsia, na shughuli.

Vitamini na Madini

• Vitamini husaidia mwili kugeuza chakula kuwa nishati na tishu.
• Kuna aina 13 za vitamini kwa ujumla: Vitamini A; vitamini B; vitamini B mchanganyiko
unayojumuisha vitamini B1, Vitamini B2, Viamnini B3 vitamin, B6, Vitamini C, Vitamin
B12 tindikali ya pantotheniki (pantothenic acid), na biotini (biotin); na vitamini C, D, E,
na K.
• Madini yanahitajika katika ukuaji na utunzaji wa miundo ya mwili. Yanahitajika pia
katika kutunza juisi za uyeyushaji chakula na mimiminiko iliyopo ndani na
kandokando mwa seli.
• Madini hayatokani na mimea wala wanyama. Mimea hupata madini kutokana na maji
au udongo, na wanyama hupata madini kwa kula mimea au wanyama wanaokula
mimea.
• Vitamini na madini hujulikana pia kama vyakula vya ujenzi na ulinzi wa mwili.
• Vijirutubishi ambavyo havipatikani kwa wingi na ambavyo husababisha matatizo
mengi yatokanayo na utapiamlo wa ukosefu wa vijirutubish duniani ni kama
vifuatavyo; madini ya joto, zinki, vitamini A, chuma na folate.

Vyanzo vya Vitamini na Madini

• Mboga jamii ya machungwa, kama vile viazi vitamu vya njano na karoti, matunda jamii
ya machungwa kama vile, embe, papai, na mawese mekundu ni vyanzo vizuri sana
vya vitamini A.
• Matunda mengi yatokanayo na jamii ya michungwa na mboga zisizoivishwa sana
huwa na vitamini C.
• Mboga za kijani kibichi hutupatia folate na kiasi cha vitamini A.
• Mbogamboga nyingi (mf. nyanya, vitunguu) hutoa vijirutubishi muhimu vya nyongeza
viwezavyo kukinga mwili dhidi ya magonjwa sugu kama ya mioyo.
• Njia bora ya kuhakikisha tunapata vijirutubishi na ufumwele wa kutosha ni kula aina
mbalimbali za mbogamboga, matunda na nafaka zisizokobolewa kila siku.
• Nyama, viungo vya ndani vya wanyama na maini ya aina zote ni chanzo kizuri sana
cha vitamini A.

Mahitaji ya vitamin na madini mwilini

• Vitamini na madini vinahitajika kwa viwango vidogo vidogo.
• Mahitaji hutegemea umri, jinsi na kiwango cha shughuli, na ulaji wa aina mbalimbali
za matunda, mbogamboga na nafaka zisizokobolewa.

Maji

Maji ni kirutubishi muhimu sana. Hakika, zaidi ya nusu ya mwili ni maji. Unaweza kuishi bila
ya chakula kwa wiki kadhaa, bali hauwezi kuishi zaidi ya wiki moja bila ya maji.
Mwili unahitaji maji ili kufanya kazi.

Umuhimu wa maji mwilini

• Kuhifadhi joto la mwili;
• Kusafirisha virutubishi mwilini;
• Kuvifanya viungo viwe na unyevunyevu;
• Kuyeyusha chakula;
• Kuondoa uchafu mwilini;
• Kupoza mwili.
(Fikiria matumizi ya maji unapojenga nyumba; bila ya maji: saruji, mchanga na zege
havitakuwa na matumizi yeyote).

Vyanzo vya maji mwilini

• Maji yenyewe
• Juisi za matunda
• Supu
• Maziwa
• Uji
• Vinywaji visivyo na kafeini (vinywaji vyenye kafeini na kileo vina madawa ya
kuongeza mkojo (diuretics) inayosababisha upotevu wa maji mwilini)

Mahitaji ya maji mwilini

Lita 1.5 au glasi 8 kwa siku.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu; Virutubishi, kazi zake katika mwili na vyanzo vyake.💯✔ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!👍

📚Msomaji wangu mpendwa, leo nimekuandalia 📖 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 ambacho nakupa kwa bei ya punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 2500/= kwa leo tuu!🙉🙉🙉 👉<<Bofya hapa Kuoda>>👈 ili nikutumie kwenye📧 email yako Leo Leo☑ Usikubali Kukosa.👍💪

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-🙉

happy-spring-smiley-emoticon.gif

.

MBINU-YA-KILIMO-BORA-CHA-MBOGA.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 2500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 kwa Tsh 2500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

vichekesho.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 6500/= hadi Tsh 2500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ kwa Tsh 2500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

📰 Posti nyingine👇

📌 Mapishi ya samaki aina ya salmon

Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.

👋soma zaidi kuhusu👉Mapishi ya samaki aina ya salmon

📌 Jinsi ya kupika Visheti

Viamba upishi

Unga 2 Vikombe

Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu

Maziwa ¾ Kikombe

Iliki Kiasi

Mafuta ya kukarangia Kiasi

Shira

Sukari 1 Kikombe

Maji ¾ Kikombe

Vanila ½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda) Kiasi

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika Visheti

📌 Vyakula vinavyoongoza kuongeza akili kwenye ubongo

BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.

👋soma zaidi kuhusu👉Vyakula vinavyoongoza kuongeza akili kwenye ubongo

📌 Matumizi ya mbaazi kama dawa

Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza kutumika kama dawa kwa kutumia majani, mizizi na maua

👋soma zaidi kuhusu👉Matumizi ya mbaazi kama dawa

📌 Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

*SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO. JIHADHARI NA ONYEKA!.*
Raia wa Ghana wanazidi kufa kwa matokeo ya ugonjwa wa Figo.
*JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
*2. Kula Chumvi kupita kiasi.* Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.
*3. Kula nyama kupita kiasi.*
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4. *Unywaji mwingi wa "Caffeins".*
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
*5. Kutokunywa maji.*
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. *** Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha: Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
*6. Kuchelewa matibabu.*
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara. Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe… Shirikisha wengine, kama unajali. ----
*Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:*
D- baridi*
Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
MWISHO… Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
*Inaweza kumsaidia mtu!*
Wasambazie wengi kwa kadiri uwezavyo.
Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.
*Maonyo muhimu ya Afya*
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa zako kwa maji baridi….
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako….!!.

👋soma zaidi kuhusu👉Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

📌 Madhara ya nyama nyekundu kwa mtu mwenye VVU

Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu

👋soma zaidi kuhusu👉Madhara ya nyama nyekundu kwa mtu mwenye VVU

📌 Jinsi ya kupika pizza ya mboga mboga na cheese

1 kilo unga wa ngano
240 ml maji ya vugu vugu
2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kidogo cha chai
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika pizza ya mboga mboga na cheese

📌 Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

Nyanya 1 kg
Maji Iita ½
Chumvi kijiko kidogo 1
Sukari

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

📌 Ushauri kuhusu mwili wako

Nimekutana na hiki kitabu japo nimekipitia juu juu nikaona nisiwe mchoyo Wa kukushirikisha wewe utakayependezwa na kusoma hapa Chini japo ni changamoto sana kwa sisi waongo kusoma

👋soma zaidi kuhusu👉Ushauri kuhusu mwili wako

📌 Tiba kwa kutumia maji

⭕Tiba kwa kutumia maji⭕
💧💧💧💧💧💧💧💧💧

👋soma zaidi kuhusu👉Tiba kwa kutumia maji
happy-bunny-smiley-emoticon.gif

📓 Posti za sasa👇

A Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

Mchele (Basmati) 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe 1 kg

Pilipili boga 1 kubwa

Nyanya 2 kubwa

Vitunguu maji 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Ndimu 1

Mafuta ya kupikia ½ kikombe

Mdalasini ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ½ Kijiko cha chai

Hiliki ½ Kijiko cha chai

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya

A MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali .Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki.

👋soma zaidi kuhusu👉MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

A Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

*SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO. JIHADHARI NA ONYEKA!.*
Raia wa Ghana wanazidi kufa kwa matokeo ya ugonjwa wa Figo.
*JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
*2. Kula Chumvi kupita kiasi.* Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.
*3. Kula nyama kupita kiasi.*
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4. *Unywaji mwingi wa "Caffeins".*
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
*5. Kutokunywa maji.*
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. *** Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha: Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
*6. Kuchelewa matibabu.*
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara. Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe… Shirikisha wengine, kama unajali. ----
*Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:*
D- baridi*
Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
MWISHO… Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
*Inaweza kumsaidia mtu!*
Wasambazie wengi kwa kadiri uwezavyo.
Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.
*Maonyo muhimu ya Afya*
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa zako kwa maji baridi….
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako….!!.

👋soma zaidi kuhusu👉Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

A Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

Wapendwa, napenda kushirikiana na nyinyi kujuzana hili nililolisikia kupitia channel ten leo asubuhi kuhusu ugonjwa wa kisukari.
Wataalam waliokua wakitoa mada walikua Prof Endrew Swai na Dr Mohamed Juma.
Kwa ufupi wamesisitiza sana kufanya mazoezi kwa takriban nusu saa kwa siku na ambayo mtu anatoa jasho na moyo kumwenda mbio. Hiyo ni kwa ajili ya kusaidia misuli ya miguu,tumbo kifua, mgongo na mikono kutumia kiasi cha sukari kinachozalishwa mwilini.
Kadhalika wamesisitiza sana kula vyakula visivyokobolewa,ikiwamo kula dona badala ya sembe,ulezi,mtama na matunda.
Watu wapunguze na ikiwezekana kuacha kunywa vimiminika vyenye sukari,ikiwamo juice,soda pombe na vinginevyo. Na hiyo nikwasababu vinywaji hivyo havikai tumboni na badala yake huenda moja kwa moja kwenye utumbo mwembamba na kulazimisha kongosho linalozalisha kemikali ya insulin kufanya kazi kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo kawaida.
Vyakula visivyokobolewa vinafaida sana kwani vinachukua muda wa kutosha kutoka kwenye tumbo na kwenda kwenye utumbo mwembamba na hatimaye kuvunjwavunjwa kwa ajili ya kutumika mwilini. Kadhalika makapi yatokanayo na hivyo vyakula hutuzuia kupata kansa ya utumbo. La ajabu wametoa takwimu za kutisha kwani ulaya kwasababu wanakula vyakula vilivyokobolewa wanapata kansa ya utumbo kuliko nchi au bara la afrika,
na kansa hiyo ni ya nne kwa kusababisha vifo barani ulaya na amerika.
Tafadhalini tujihadharini kwani mada ilikua ndefu na nzuri sana kwa mustakabali wetu na afya zetu.
1.Mazoezi ni muhimu
2.Vyakula viwe na uasilia wake
3.Mtu aliye na mwenza wake afanye tendo la ndoa kwa kadiri inavyowezekana kwani ni sehemu ya mazoezi
4. Tubadili mifumo ya maisha yetu,kukaa tu bila kuishughulisha miili yetu.
Atakayeona anataka kupata elimu zaidi hao madaktari niliowataja wapo hospitali ya muhimbili kitengo cha tiba ya kisukari.
Ufahamu juu ya afya yako binafsi …nimeikuta sehemu 👆👆👆👆👆👆

👋soma zaidi kuhusu👉Dondoo Muhimu kuhusu ugonjwa wa kisukari

A Jinsi ya kuepuka kunuka mdomo

JINSI YA KUEPUKA KUNUKA MDOMO
MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kuepuka kunuka mdomo

A Jinsi ya kupika Mgagani

Mgagani mkono 1
Mafuta vijiko vikubwa 4
Karanga zilizosagwa kikombe ½
Maji kikombe 1
Kitunguu 1
Karoti 2
Maziwa kikombe 1
Chumvi kiasi

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika Mgagani

A Ushauri kuhusu mwili wako

Nimekutana na hiki kitabu japo nimekipitia juu juu nikaona nisiwe mchoyo Wa kukushirikisha wewe utakayependezwa na kusoma hapa Chini japo ni changamoto sana kwa sisi waongo kusoma

👋soma zaidi kuhusu👉Ushauri kuhusu mwili wako

A Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

Kumekuwepo na tatizo la vifo vya ghafla sana tena kwa watu ambao wana afya njema na hii inatokana na kuamka ghafla usiku ambapo ubongo hukisa damu ya kutosha.

👋soma zaidi kuhusu👉Dondoo muhimu kwa Afya yako unapostuka usiku

A Jinsi ya kupika Keki Ya Maboga

Unga wa ngano vikombe vikubwa 3
Boga lililopondwa kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Sukari kikombe kikubwa 1
Blue band kikombe ½
Vanilla kijiko kidogo 1
Mayai 2
Maji kiasi/ maziwa
(kama nilazima)

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika Keki Ya Maboga

A Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

Nyanya 1 kg
Maji Iita ½
Chumvi kijiko kidogo 1
Sukari

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya
clicking-your-heels-smiley-emoticon.gif

Majarida na vitabu kutoka Ackyshine eBook Shop

MBINU-YA-KILIMO-BORA-CHA-MBOGA.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 7000/= hadi Tsh 2500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 kwa Tsh 2500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

vichekesho.jpg
Kwa punguzo kutoka Tsh 6500/= hadi Tsh 2500/= kwa leo tuu!.
Jipatie 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ kwa Tsh 2500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

happy-bunny-smiley-emoticon.gif
happy-spring-smiley-emoticon.gif