Umuhimu wa kupata chanjo

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba, ni vyema mtu ukachukua tahadhari mapema kabla haujafikwa na jambo au tatizo fulani.

Vivyo hivyo katika chanjo, hii ni kinga ambayo hutolewa kwa binadamu na katika umri tofauti tofauti ili kuuwezesha mwili kutengeneza ulinzi asilia (antibodies) ambao utauwezesha mwili uwe na nguvu zaidi za kupambana na magonjwa au visababishi vya matatizo mbalimbali ya kiafya ambavyo siku zote vimekuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.

Mpenzi msomaji, ni vyema ukafahamu kuwa chanjo SIYO tiba, na siku zote hutolewa kwa watu ambao hawana ugonjwa au tatizo husika linaloendana na chanjo hiyo, mfano, kama mtoto anao ugonjwa wa surua, basi itabidi apate matibabu ya surua na siyo chanjo ya surua. (Ila kumbuka kuwa matatizo mengine ya kiafya kama vile kukohoa, kuharisha au mafua, havimzuii mtu kupata chanjo).

Pengine utajihoji ni kwa nini inakuwa hivi?, hii ni kutokana na kwamba, chanjo siku zote dozi za dawa zake huwa ni kidogo ukilinganisha na dozi endapo hiyo dawa itatumika kutibu ugonjwa husika mfano surua au kifua kikuu, hivyo kwa kuwa dozi ni ndogo, basi haitakuwa rahisi kutibu mtu ambaye tayari anao ugonjwa.

Kitu kingine katika chanjo ni kwamba, baadhi ya chanjo huwa ni chembe chembe maalumu ambazo hufanana na aina ya ugonjwa ambao umekusudiwa kuzuiliwa au kukingwa, hivyo chembe chembe hizi huwa katika kiwango kidogo sana ambacho hakiwezi kukusababishia matatizo yoyote ya kiafya, ila mwili wako utaamshwa utengeneze kinga za kutosha ili endapo mazingira uliyopo yatakuwa na ugonjwa huo husika, wewe mwili wako utakuwa tayari kupambana ila chembe chembe hizi maalumu hazitaweza kukutibu endapo tayari unao ugonjwa husika.

Mambo ambayo huweza kujitokeza baada ya mtu kupata chanjo ni pamoja na hali ya joto la mwili kupanda au homa, ingawaje siyo lazima mtu apatwe na hali hiyo cha kufanya ni kutumia dawa za kushusha homa na baada ya muda mwili wako utarejea katika hali yake ya kawaida, hivyo endapo hali hiyo itajitokeza kwako usiwe na shaka.

Chanjo itakuwezesha kujikinga dhidi ya magonjwa, kukupunguzia gharama za matibabu na utapata muda ya kuendelea na shughuli zako za kila siku, kwani wewe au familia yako mtakuwa na afya bora.


elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Umuhimu wa kupata chanjo;

a.gif Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe… endelea kusoma

a.gif Vyakula vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu. Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni vyakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya mwili wako.. endelea kusoma

a.gif Aina ya mazoezi na umuhimu wa mazoezi kwa wamama wajawazito

Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake… endelea kusoma

a.gif Chanzo, dalili, aina na matibabu ya ugonjwa wa kifafa

Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara… endelea kusoma

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

[Kichekesho Kwako] 👉Angalia huyu polisi kitu alichonijibu

picha-kali.png

a.gif Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Viazi utamu 3
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu
Tango
Limao
Chumvi
Pilipili
Mafuta (vegetable oil).. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Unga wa ngano 1 Kilo.. endelea kusoma

a.gif Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Supu Ya Maboga

Blue band vijiko vikubwa 2
Maziwa vikombe 2
Royco kijiko kikubwa 1-2
Pilipili manga (unga) kijiko cha 1
Chumvi kiasi Maji lita 2-3
Boga kipande ½
Viazi mviringo 2
Vitunguu 2
Karoti 2
Nyanya 2.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Ushauri kwa mtu

[Jarida la Bure] 👉Picha Kali Za Kuchekesha

afya-mapishi-na-lishe.png

.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png
uliyesoma.gif
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.