Umuhimu wa kula fenesi kiafya

By, Melkisedeck Shine.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.

Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutub
isho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.

Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.

Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.

Wataalamu wa mambo ya afya wamezitaja faida nyingine za tunda hili kuwa ni pamoja na:

Kinga:

Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.

Nishati:

Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.

Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Asthma:

Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Umuhimu wa kula fenesi kiafya;

a.gif Jinsi ya kufanya kupunguza mwili kwa kupanga ulaji wa chakula

Ulaji wa vyakula vingi vya wanga na mafuta ni chanzo kikubwa cha unene na uzito kuongezeka. Vyakula kama ugali,wali,mkate mweupe,bia na pombe za kienyeji zinazotokana na wanga (kimea) huchangia kuongezeka kwa uzito. Matumizi ya aina hii ya chakula ni muhimu kupunguzwa katika mlo wako… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa Dakitari

Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari. Kutokana na uwepo wa maduka ya dawa baridi, watu wengi wanapojisikia kuwa wagonjwa, hununua dawa kwenye maduka hayo na kuanza kuzitumia… endelea kusoma

a.gif Mwanamke kuamka mapeme asubuhi kunapunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti

Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti… endelea kusoma

a.gif Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo… endelea kusoma

a.gif Dalili za homa ya dengu (Dengue fever)

Dengue ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia papai

Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili ya urembo hasa kwa wanawake… endelea kusoma

a.gif Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Unaweza kutibu chunusi bila kwenda hospitalini kama ifuatavyo;.. endelea kusoma

a.gif Faida za kula Tende kiafya

Zifutazo ni faida zitokanazo na ulaji wa tende;.. endelea kusoma

picha-kali.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
NIMEKUMISI-MPENZI086H.JPG
familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.