Soma hii Kabla hujafikiria kula nyama ya nguruwe tena

By, Melkisedeck Shine.

JEE NYAMA YA NGURUWE (KITI MOTO) NI SALAMA KWA BINADAMU???

Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu wa MEDICINE (Science)!!

Nguruwe ni mnyama anaeliwa na 38% ya watu wote duniani Na walaji wake ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Europe, Sub-Saharan Africa, America ya kaskazini , kusini mwa America, na Oceania.

Nguruwe ni mnyama ambae, Ana umbo la pekee sana, tukiangalia kuhusu madhara yake au faida yake , tunangalia vitu vinavyopatikana ktk mwili wake, tukilinganisha Na Faida.

FAIDA ZA NYAMA YA NGURUWE KITAALAMU

👉🏾Kunapatikna vitamini muhimu ktk mwili Wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12
👉🏾Unapata madini ya Chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
👉🏾Nyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako Na kuifanya iwe laini.
👉🏾Nyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida ktk mwili Wa binadamu
👉🏾Nyama ya nguruwe ina protein ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili
👉🏾Nyama ya nguruwe ina mafuta ambayo hutupa nguvu mwilini

HASARA YA NYAMA YA NGURUWE

Licha ya faida tajwa hapo juu, vile vile kuna hasara ya kutumia nyama hii.
👉🏾Nyama ya nguruwe ; ina sumu ya carcinogen ambayo inasababisha kansa; kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Na shirika la afya duniani ( WHO), Na The International Agency for Research on Cancer!! Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku 50gms basi uwezekano Wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa 18%
👉🏾Anasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na Centers for Disease Control and Prevention inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 ambaye anatokana Na Nguruwe(kiti moto) imeripotiwa kusababisha maradhi ya mripuko kwa nchi za MAREKANI
👉🏾Nyama ya nguruwe ina minyoo wajulilanao kwa jina la trichinella worm , ambao wadudu hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa joto Hata la 100C , utafiti uliofanyika 1998 Na WHO ukaonesha nyama ya Nguruwe iliopikwa kwa Joto la 104C , Huwa asilimia 52.37% ya trichinella worm wanabaki kuwa hai!! Wadudu hao wakiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; ambao huwa Na dalili kama ifuatavyo:
✅Homa kali sana
✅Kichwa kuuma
✅Kukosa nguvu
✅Maumivu ya nyama za mwili
✅Macho kuwa rangi ya pink(conjunctivitis)
✅Kuvimba uso Na kope
✅Kudhuriwa Na mwanga
👉🏾Nyama ya nguruwe ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambaye husababisha homa ya ini aina E
👉🏾Wadudu wengine ni kama;
🥄Nipah virus
🥄Menangle virus
🥄Viruses Ktk kundi Paramyxoviridae
Ambao wote hao; huwa wanaleta madhara kwa mwili Wa binadamu!!
👉🏾Nyama ya nguruwe husababisha Maradhi ambayo Yana resistance(ukinzani) Na ANTIBIOTICS
👉🏾Nyama ya nguruwe ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu ya shirika la Afya duniani(WHO) - Reference….open_http://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/taeniasis-cysticercosis
Wanasema; minyoo hii huwa;
👉Unaweza kuipata ikiwa hautapika nyama vizuri au Ukila nyama ya kuruwe ilioathirika(infected): Kwa hyo sio kila nyama ya Nguruwe iliopikwa vizuri, huwezi kupata minyoo hii.
👉Minyoo hii ikiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo Wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis
Mfano wake ni kifafa
👉30% ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa Na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe
👉🏾Watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa , huwa ni walaji wazuuri Wa Nguruwe.

JEE NG'OMBE, MBUZI, KONDOO NA WANYAMA WENGINE WALIWAO NA WENGI HAWANA MINYOO??

Ukweli ni kwamba Hata wanyama wengine nyama zao huwa zina minyoo aina ya Taenia saginata.
Ila minyoo ya Taenia saginata ni tofauti Na Taenia solium kwa sababu; Saginata wanakufa kwa joto Dogo sana, lakini solium wanahitaji 71C bila Hata kupungua!!
Swali langu kwako wewe msomaji Wa nakala hii;
👉🏾Nani anaepika huku akipima joto limefika au laa???

HITIMISHO

Tahadhari, sana Na nyama ya nguruwe , kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake!!!

Shared from;
Dr Isack

[kitendawili kwako] 👉Hazikauki umande

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Soma hii Kabla hujafikiria kula nyama ya nguruwe tena;

a.gif Faida za mafuta ya nazi kiafya kwenye mwili

Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’enywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama ‘ketones’… endelea kusoma

a.gif Faida za kufanya Masaji kiafya

Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama ‘cytokines’ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama ‘cortisol’… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuondoa kitambi na kupata afya nzuri

☘☘piga chini kitambi☘☘.. endelea kusoma

UJUMBE-POLE-NDUGU.JPG

a.gif Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes… endelea kusoma

a.gif Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutengeneza Nangatai

Unga wa ngano - 2 - 2 ¼ Vikombe.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuandaa Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi

Nyama Ya Mbuzi - 1 Kilo.. endelea kusoma

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

KADI-POLE-MZAZI.JPG
SALAMU-JIONI98HBS.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.