Sababu ya meno kubadilika rangi

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe.

Meno kubadilika rangi huweza kuwa ni sababu moja au muunganiko wa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;

Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye kaboni, sigara na mvinyo (wine) kwa muda mrefu husababisha kubadilika kwa rangi ya meno kwa juu (extrinsic staining).

Utumiaji wa maji yenye madini mengi ya fluoride katika kipindi cha utoto (dental fluorosis).

Matumizi ya dawa aina ya tetracycline kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayapata madini ya kutosha.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ya juu ya jino (amelogenesis imperfecta). Iwapo sehemu hii imeumbwa ikiwa laini kuliko inavyotakiwa huwa rahisi kufyonza rangi na jino huota likiwa limebadilika rangi au hubadilika baada ya muda.

Kufa kwa sehemu hai ya jino hasa kutokana na kuumia kwa jino au ajali (pulp necrosis), hali hii huweza huchukua miaka mingi mpaka kutokea kubalika rangi ya jino..

Jino liliozibwa kwa kutumia material aina ya amalgam huweza kubadilika rangi na kuwa nyeusi.

Mara nyingne jino lililotibiwa kwenye mzizi wa jino (root canal treatment ) huweza kubadilika rangi baada ya miaka mingi.

Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika kuyafanya meno yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kuwa meupe.

Njia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na jinsi alivyoathirika. Kuna njia nyingi ambazo huweza kuyang’arisha kwa ndani (internal bleaching) au kuyangarisha kwa nje (external bleaching).

Endapo una tatizo la meno yaliyobadilika rangi, muone daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu kwani kinywa kizuri na chenye afya huongeza kujiamini.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Sababu ya meno kubadilika rangi;

a.gif Vyakula vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili

Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu. Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni vyakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya mwili wako.. endelea kusoma

a.gif Vyakula visivyotakiwa kipindi cha ujauzito

Ili mtoto azaliwe akiwa na afya njema pamoja na akili timamu, akiwa tumboni lazima alishwe lishe bora na mlo sahihi. Mwenye jukumu la kutoa lishe bora na sahihi kwa kiumbe kilichomo tumboni ni mama. Anatakiwa kujua aina ya vyakula anavyopaswa kula. Vivyo hivyo, anatakiwa kujua aina ya vyakula vya kuviepuka… endelea kusoma

a.gif Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba, ni vyema mtu ukachukua tahadhari mapema kabla haujafikwa na jambo au tatizo fulani… endelea kusoma

a.gif Aina ya mazoezi na umuhimu wa mazoezi kwa wamama wajawazito

Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake… endelea kusoma

a.gif Aina ya mazoezi na umuhimu wa mazoezi kwa wamama wajawazito

Leo tutaongelea mazoezi gani ya kawaida ambayo mama mjamzito anaweza kuendelea kuyafanya kila siku ya ujauzito wake na umuhimu wake… endelea kusoma

a.gif Mbinu 11 za kufuata ili uweze kuacha pombe

Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia. Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

 1. Mchele (Basmati) - 3 vikombe
 2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) - 1 kikombe
 3. Kuku Kidari - 1 LB (ratili)
 4. Mayai - 2 mayai
 5. Vitunguu (vikubwa) - 2 au 3 vidogo
 6. Pili pili manga - 1 kijiko cha chai
 7. Paprika - 1 kijiko cha chai
 8. Chumvi - Kiasi
 9. Mafuta - 1/3 kikombe cha chai
 10. Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha supu
 11. Tangawizi - 1 kijiko cha chai
 12. Kidonge cha supu - 1
 13. Soy sauce - 2 vijiko vya supu.. endelea kusoma

a.gif Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku… endelea kusoma

afya-mapishi-na-lishe.png

.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png
Slide1-mabest-skull.PNG
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.