Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo

Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi sana katika dunia, watu wamekuwa wakiteseka bila kujua nini chanzo cha tatizo hili na vipi kuliondoa tatizo hili na wengine wamekuwa wakilipuuzia bila kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kutokana na tatizo hili.

Tatizo hili hutokea pale mtu anakula vizuri lakini unakata siku tatu hadi nne bila kupata choo. Ukiona unakula kutwa mara tatu na unakaa siku mbili hadi tatu huendi chooni au unatoa choo kigumu kama mbuzi hilo ni tatizo kwako.

Tafiti zinaonyesha mtu anaweza kupoteza maisha kama atakosa choo kwa siku tano hadi saba mfululizo.Watu wengi hulidharau tatizo hili lakini linamadhara makubwa tofauti na wanavyofikiria.

Zifuatazo ndizo sababu za kukosa choo;

 • Kupenda kula saana vyakula vilivyokobolewa (mfano ugali wa sembe,mikate n.k)
 • Ukosefu wa mbogamboga za majani na matunda ya faiba kama machungwa,ukosefu wa kula mboga za majani na matunda hasa ya faiba kama machungwa huongeza tatizo hili.kila mtu anatakiwa kula matunda aina mbili na mboga za majani aina mbili kila siku.
 • Matumizi makubwa ya pombe na sigara
 • Unywaji mdogo wa maji. Kila mtu anapaswa kunywa maji kwa kiwango cha chini lita 3 kila siku na usinywe maji wakati unakula, kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula.
 • Matumizi mabaya ya madawa. Mfano dawa za presha, aleji n,k.
 • Kuugua kisukari au ugonjwa wa misuli.
 • Kansa ya utumbo mpana

Yafuatayo ndiyo madhara yatokanayo na kokosa choo;

 1. Unaweza kuugua saratani ya utumbo mpana.
 2. Unaweza kupata tatizo la tumbo kujaa gesi.
 3. Figo yako inaweza isifanye kazi vizuri.
 4. Unawezasababisha magonjwa ya moyo.
 5. Unaweza pata tatizo la kukakamaa mishipa ya damu ambapo utasababisha miguu kuwaka moto na ganzi miguuni au mikononi.
 6. Unawezasababisha magonjwa ya ini
 7. Unawezapata kisukari


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Sababu na madhara ya tatizo la kukosa choo;

a.gif Faida za kula Karoti kiafya

Asilimia kubwa tunapenda kutumia karoti katika kuunga katika mboga ya nyama na si kuila karoti kama karoti. wataalamu wanashauri ili uwe na afya bora unatakiwa ule karoti sita kwa wiki au moja kwa siku. Unaweza kula karoti ya kuchemshaa,juisi au mbichi… endelea kusoma

a.gif Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction)… endelea kusoma

a.gif Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu wa kati mita 9 hadi 18 na huanza kuzaa matunda ukiwa na miaka 6 na kuendelea kwa miaka zaidi ya 50… endelea kusoma

a.gif Faida za kula karanga mbichi

Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya… endelea kusoma

a.gif MADHARA YA SHISHA

Yafuatayo ni madhara ya shisha;.. endelea kusoma

a.gif Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu

Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu… endelea kusoma

a.gif Umuhimu wa kula fenesi kiafya

Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu… endelea kusoma

a.gif Vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kutumia

Vipo vitu mbalimbali ambavyo mama mjamzito hapaswi kuvitumia wakati wa ujauzito kwani vina athari kubwa sana kwake yeye mwenyewe pamoja na mwanaye aliye tumboni… endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png
SALAMU-JIONI98HBS.JPG
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.