Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

By, Melkisedeck Shine.

vichekesho-bomba-vya-siku.png

Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu.

Kiungulia ni nini?

Kiungulia ni maumivu mithili ya moto yanayotokea kifuani sehemu ya katikat ya kifua. Maumivu haya hayana uhusiano na moyo.Yanatokea pale asidi ya kwenye tumbo inapopanda na kurudi kwenye koo la chakula.

Asidi hii ikiwa tumboni haisababishi madhara wala maumivu kwani inazalishwa muda wote na kuta za tumbo kumeng'enya chakula. Seli za kuta za tumbo haziathiriki na asidi hii ndio maana inapokuwa tumboni haileti shida yoyote.
Ila seli za kuta za koo la chakula haziwez kustahimili asidi hii ndiyo maana inapopanda kwenye koo la chakula unapata maumivu ya kiungulia.

Dalili ya kiungulia

Kiungulia mara nyingi hutokea wakati unakula au baada ya kula na kinaweza kuzidi makali wakati umelala.

Dalili ni kama, Kuhisi maumivu kama ya kuungua kwenye kifua au chembe moyopamoja na kujisikia radha ya uchachu mdomoni.

Saabu za kiungulia kwa wajawazito.

Sehemu mbali mbali za mwili hupata mabadiliko wakati wa ujauzito. Wakati wa ujauzito mwili hutengeneza kwa wingi hormone ya progesterone na relaxin ambazo huathiri mfumo wa chakula.

Progesterone hormone hii hufanya chakula kutembea na kufyonzwa kwa taratibu sana.
Relaxin hormone hufanya misuli laini ya mwili kulegea ikiwemo misuli inayobana sehemu ya juu ya tumbo (sphincter) inayozuia chakula au vitu vya tumboni visirudi kwenye koo la chakula .
Mabadiliko haya hufanya kuwa rahisi asidi na chakula vilivyomo tumboni kurudi kwenye koo la chakula na kusababisha kiungulia.

Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kiungulia kwa mama mjauzito ni;

 1. Kula chakula kingi sana
 2. Vyakula vyenye viungo
 3. Vyakula vyenye mafuta mengi
 4. Matunda jamii ya limao na machungwa
 5. Chocolate
 6. Soda
 7. Kahawa
 8. Sigara
 9. Pombe
 10. Baadhi ya madawa
 11. Stress
 12. Uzito uliopitiliza.

Jinsi ya kujikinga na kiungulia kwa wajawazito.

 1. Kuwa na uzito unaowiana na urefu wako
 2. Epuka vyakula vinavyosababisha kiungulia kama nilivyoainisha hapo juu
 3. Epuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja. Bali kula chakula kidogo kila baada ya muda.
 4. Kunywa maji ya kutosha. Angalau lita moja na zaidi kwa siku
 5. Epuka kuvaa nguo zinazobana sana tumbo na kiuno
 6. Usilale muda mfupi baada ya kula.
 7. Epuka kuwa na msongo wa mawazo /stress
 8. Onana na Daktari kupata ushauri wa dawa za kupunguza makali ya asidi hii ambazo ni salama kwa wajawazito


vichekesho-bomba-vya-siku.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito;

a.gif Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)

Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes… endelea kusoma

a.gif Dalili za kuharibika kwa Mimba

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Sababu kuu huwa ni magonjwa kama vile ugonjwa hatari wa malaria, ugonjwa unaotokana na zinaa kama vile kaswende na kisonono na U.T.I, dawa fulani fulani mfano Albendazole, Misoprostol, Metronidazole na kadhalika… endelea kusoma

a.gif Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu. Tunda hilo ambalo kwa umbo linafanana na tufaa (apple), lina faida nyingi kwa binadamu iwapo atalitumia mara kwa mara… endelea kusoma

[Video Nzuri] 👉Uhesabuji wa hela wa kiajabu

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

a.gif Jinsi ya kufanya ili upate mtoto wa kike au wa kiume

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana.. endelea kusoma

a.gif Mapishi ya tambi za kukaanga

Kupika tambi ni kama ifuatavyo.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kupika Wali wa hoho

Wali wa hoho ni chakula maalum kinachotumika katika hafla au sherehe. Ni chakula chenye ladha nzuri na kina muonekano wa kuvutia kinapokuwa mezani tayari kwa kuliwa… endelea kusoma

a.gif Mapishi ya Tende Ya Kusonga Ya Lozi Na Cornflakes

Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Kushindwa jambo sio Makosa

[SMS kwa Umpendaye] 👉Ujumbe mzuri kwa umpendaye

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png
KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.